Tuesday, December 15, 2020

KUZOROTA UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME LEMUGURU KWASABABISHA WAZIRI WA NISHATI KUTOA MAAGIZO KWA MKANDARASI,TANESCO


Waziri wa nishati Dkt . Medard Kalemani katikati akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kituo chakipoozea umeme Kv 400 Lemuguru kilichopo Ndani ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha alipotembelea Mradi huo leo (Jana) na kuangalia Mradi huo ulipofikia ambapo aliwataka wafanye kazi usiku na mchana adi ifikapo March  31 ,2021 Mradi huo uwe umekamilika.(picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)


Na Woinde Shizza ,ARUSHA

WAZIRI  wa Nishati  Dkt. Medard  Kalemani amechukizwa na kitendo cha kuzorota kwa mradi  wa kituo cha kupozea umeme kilichopo Lemuguru katika Kata ya Matevesi wilayani Arumeru mkoani Arusha 

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo Dkt .Kalemani ametoa muda wa

miezi mitatu kwa mkandarasi wa kampuni ya consortium Energoinvest &E.M.C LTD ,Irfan Djovic Kuhakikisha nradi huo unakamilika kwa muda huo aliowapa.

Amesema mradi huo ulianza  Desemba mwaka 2017 na ulitakiwa ukamilike ndani ya miaka mitatu, lakini shughuli za ujenzi rasmi zilinza rasmi  mwaka 2018.Gharama  za mradi huo ni Dola milioni 258.2 na unajegwa umbali wa kilometa 414 kwa Tanzania na mpaka kufikia upande wa Kenya Naisinyai itakuwa imefikia kilometa 512 huku ikielezwa laini hiyo ni muhimu kwa nchi yetu mpaka nchi za jirani.

Dk.Kalemani ameongeza  mradi huo ulitakiwa ukamilike Desemba 31 mwaka huu lakini baada ya kuutembelea  ameona mradi huo hauta kamilika kwa wakati huo.Akiwa katika mradi huo mkandarasi wa ujenzi huo ametoa sababu mbalimbali ikiwemo janga la Corona na mvua ,madai ambayo Waziri ameyakata na kueleza nchini kwetu hakuna Corona.

"Nielekeze  wafanyakazi waongezwe , pia mkandarasi zile mashine kubwa ambazo zinaagizwa nje kwa ajili ya kituo hichi Cha kupozea umeme mkandarasi ulitaka  uanze kuleta vifaa hivyo mwezi Januari , mimi  ninakwambia hapana anza  kuingiza  kesho hivyo vifaa ili  mpaka Januarii  viwe vimefika hapa na Mradi huu mhakikishe  unakamilika nwishoni mwa Machi, "amesema.

Aidha amemtaka Meneja wa Mradi  huo pamoja msaidizi wake ambaye ni Mhandisi ampeleke maelezo ndani ya siku tatu  kwanini mradi huo umesimama na wafanyakazi hawapo  kazini mpaka Sasa na kwanini haujakamilika kwa wakati  na maelezo hayo  akiyasoma asipo rizika nayo inawabidi wajiuzuru.

Dk.Kalemani amemtaka meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha Hereni Mhina pamoja na  Meneja wa Shirika hilo Wilaya ya Arumeru  pamoja na wa Kanda kusimamia wakandarasi wamalize mradi huo kwa wakati  ,huku akiwasisitiza  wasiende kula sikukuu mpaka pale mradi utakapo kamilika.

Pia amewasisitiza  wakandarasi wageni kutoka nchi za nje kuzileta familia zao hapa nchini nakusherekea sikukuu pamoja ili wasitafute visingizio vya kusema wanaenda kula sikuku makwao,ambapo pia aliwasisitiza wafanye kazi usiku na mchana  ili adi ifikapo mwezi March Mradi uwe umekamilika.

"Umuhimu wa Mradi huu unafanya kazi tatu kazi ya kwanza kujenga laini ya kufikisha  umeme lemuguru umbali wa kv 400 ambayo inaendana na kv 220 kazi ya pili inasambaza umeme Katika vijiji 38  ambavyo vipo  mikoa ya Singida , Manyara na Arusha kuchelewa kwake kunachelewesha wananchi ambao wapo kwenye laini kupata umeme hivyo ni vyema Mradi huu unakamilika haraka,"amesema.

Kwa upande wake Mhandisi Msimamizi wa mradi  wa kituo Cha kupozea umeme kituo cha Lemuguru  Blandina  Joachim  amesema mpaka sasa mradi umekamilika   kwa asilimia  60,na hiyo inatokana na changamoto ambazo wameziainisha lakini Waziri amezikataa.

 

No comments :

Post a Comment