KUHUSU TAARIFA YA UPOTOSHAJI KUHUSIANA NA NAFASI ZA KAZI YA UKUSANYAJI USHURU WA MAEGESHO YA VYOMBO VYA MOTO
- Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
inapenda kuujulisha UMMA wa Watanzania kuwa kumekuwepo na taarifa
zilizozua taharuki baina ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo
“Whatsapp” kuhusu nafasi ya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho ya
vyombo vya moto (Magari, Bajaji na Pikipiki) katika Mikoa ya Mwanza,
Mbeya, Arusha, Dodoma na Dar Es Salaam. Aidha, katika tangazo hilo
imeelezwa kuwa kazi hiyo itakuwa ya mkataba wa miezi sita (6) na
mshahara utakuwa kuanzia Shilingi 300,000/= kwa mwezi.
- Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
inakanusha kuhusu tangazo hilo na kuueleza UMMA kuwa wapuuze taarifa
hizo kwa kuwa hazina ukweli wowote na wala hazijatolewa na Ofisi hii,
ambayo ndio yenye dhamana ya kusimamia masuala ya Kazi.
- Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
inawataka watu wanaoeneza taarifa hizo za uongo kuacha upotoshaji huo
mara moja. Aidha, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao endapo
watabainika kukaidi maelekezo haya.
No comments :
Post a Comment