Thursday, December 31, 2020

Kilimo Cha Parachichi Chawapa Mamilioni Wakulima Njombe


***********************************

NJOMBE

Wakulima wa zao la parachichi ambalo limebatizwa jina la dhahabu ya Kijani na wakazi wa

Njombe wameongeza kasi ya uwekezaji katika kilimo hicho kinachokuwa kwa kasi ulimwenguni kwa lengo la kuja kuwa tirionea na wawekezaji wakubwa wanaochangia pato kubwa la taifa na ajira kwa vijan.

Kilimo hicho ambacho kimeanza kushika kasi mwaka 2009 baada ya halmashauri ya mji wa Njombe kuchangua zao hilo kuwa la kimkakati na kipaumbele na kuanza kuhamasisha wananchi kulima kimeyapiku mazao maarufu mkoani Njombe ikiwemo miti ya mbao na viazi kwani idadi kubwa ya wakulima wakivuna miti wanapanda parachichi kutokana na uhakika wa soko la ndani na nje.

Bruno Mwepelwa,Rozalia Mnyanga na Goden Nyava ni baadhi ya wakulima wa parachichi wanaoendesha shughuli za kilimo katika kijiji cha Maheve nje kidogo ya mji wa Njombe ambao wanasema walianza kuwekeza wakati soko likiwa la shida lakini hivi sasa kimewafanya kuwa mamilionea na kuwa na uwezo wa kuajiri vijana wengi mashambani mwao.

Mara baada ya kueleza namna kilimo hicho kilivyobadili maisha yao kutoka kwenye umasikini mkubwa na kuwa kwenye maisha ya kati ,wakulima hao wameeleza changamoto iliyopo na matarajio yao ya baadae kuwa maji tatizo na kwamba matarajio ni kuja kuwa uwekezaji mkubwa zaidi 

Lakini mafanikio makubwa ya wakulima yanatajwa kupigwa jeki na serikali ya halmashauri ya mji wa Njombe ambayo iliamua kuchagua zao la parachichi miaka ya 2000 kuwa zao la kimkakati na kipaumbele na kisha kuanza kutoa elimu na hamasa kwa wakazi kuwekeza jambo ambalo limeiongezea mapato halmashauri na kubadili maisha ya watu ,Kama ambavyo Maria Lyanzile Mtaalamu wa kitengo cha Mboga ,Maua na Viungo anavyoeleza kwamba wamefanikiwa kuunda vikundi 23 vya wakulima wa parachichi,mashamba darasa na kujenga vituo vya pamoja vya kiashara(ONE STORK CENTER)

 

No comments :

Post a Comment