Hii inakuwa mara ya kwanza hiyo ndege maarufu kurudi Amerika ya kusini tangu safari za ndege za abiria zilivyokatisha safari zake kutokana na mlipuko wa Covid-19 tangu Machi 2020. Emirates ilirudi Sao Paulo tangu Agosti 2020 na ndege yake aina ya Boeing 777-300 ER.
Abiria wanao safiri kwenda na kurudi kutoka Brazil kwenye ndege ya Emirates kuanzia Januari 2020 wataweza tena kufurahia uzoefu wa Emirates A380 isiyo na mfano na starehe ya hali ya juu, bidhaa na huduma bora.
Mwanzoni wa Novemba Emirates iliboresha huduma ya chakula katika ngazi zote za ndege wakati wakizingatia usafi na afya ya abiria na wafanyakazi. Abiria sasa wanaweza kuchagua milo tofauti tofauti pamoja na vinywaji kama mvinyo. Ufanisi wa burudani wa Emirates ndani ya ndege “ice” inaendelea kuongeza mambo mapya kila mwezi katika chaneli 4,500.
Abiria kutoka Brazil wanao safiri kwenda sehemu mbalimbali ikiwemo Maldives wanaweza kutua Dubai na kufurahia maeneo mbalimbali ya starehe kama fukwe za bahari na maonesho ya tamaduni huku Wananchi wa Brazil wanaweza kupata visa ya kuingia Dubai bure.
Mwaka 2019, Dubai ilipokea wageni milioni 16.7 na iliandaa mamia ya mikutano na maonesho, Pamoja na matukio ya michezo na burudani. Dubai ilikuwa kati ya miji ya kwanza kupata mhuri wa “Safe Travel” kutoka kwa “World Travel and Tourism Council”.
Emirates inaendelea kuongoza sekta na kurudisha imani ya kusafiri. Ilikiuwa ndege ya kwanza kuwapa matibabu ya COVID 19 wateja na hii ikawezeshwa zaidi kwa kuwapa bima, sambamba na kutoa huduma za lounge na spa.
Emirates imezindua technolojia ya biometric Dubai na nafasi ya kujihudumia na kuweka mizigo ambayo imepunguza ukaribu wa wateja na kurahisiha usafiri.
No comments :
Post a Comment