Thursday, December 31, 2020

BASHUNGWA AKUTANA NA WAFANYABIASHA WA KAYANGA NA ATOAA POLE KWA WAHANGA WA MOTO.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akiongea na wafanyabiashara wa mji wa Kayanga wakati akitoa pole kwa wahanga wa ajali ya moto uliotokea Desemba 26, 2020 uliounguza maduka kumi na kusababisha hasara ya Zaidi ya milioni mia moja tisini, katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Agaza, Kayanga, Karagwe. Leo desemba 31, 2020 (Picha zote na Eliud Rwechungura)

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (katikati) akitoa mapendekezo yatakayosaidia kukokomesha majanga ya moto wilaya Karagwe katika kikao na wafanyabiashara wa mji wa Kayanga na wahanga wa ajali ya moto kilichofanyika katika ukumbi wa Agaza, Kayanga, Karagwe. Leo desemba 31, 2020 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akikabidhi kiasi cha cha shilingi milioni moja laki mbili kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka kama mkono wa pole kwa wahanga wa ajali ya moto uliotokea Desemba 26, 2020 uliounguza maduka kumi na kusababisha hasara ya Zaidi ya milioni mia moja tisini, katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Agaza, Kayanga, Karagwe. Leo desemba 31, 2020

******************************************

Na Eliud Rwechungura- Karagwe Kagera

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na wafanyabiashara wa mji wa Kayanga na kutoa pole kwa

wahanga wa ajali ya moto uliotokea Desemba 26, 2020 uliounguza maduka kumi na kusababisha hasara ya Zaidi ya milioni mia moja tisini.

 

Mhe. Waziri Bashungwa amekutana na wafanyabiashara hao leo desemba 31, 2020 katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Angaza ulipo mji wa Kayanga, Karagwe na baada ya hapo ameambatana na wafanyabiashara wote kutembelea eneo la maduka yaliyoungua.

Mhe. Waziri Bashungwa ametoa maelezo juu ya gari la zimamoto ambapo amebainisha kuwa mpaka sasa wilaya ya Karagwe ni wilaya ya pekee yenye gari hilo lakini amekuwa akipokea taarifa kuwa gari ni bovu, jambo ambalo imemlazimu kutoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya kufanya matengenezo gari hilo haraka iwezekanavyo.

‘‘Mimi ndiye niliyepamba kupatikana kwa gari la zimamoto, ukiangalia kwenye mkoa wa Kagera, wilaya yenye gari la zimamoto ni hapa karagwe tu. Mkuu wa Wilaya ninakuamini katika uchapa kazi lakini tunapozungumzia kukomesha ajari za moto tukumbuke na kukomesha ubovu wa gari letu la zimamoto, hatuwezi kujenga fire brigade kama ya ulaya lakini tukawa na gari bovu bovu”

 

Aidha, Mhe. Waziri Bashungwa ametumia nafasi hiyo kuwaomba na kuwakumbusha wafanyabiashara wote kukata bima ya moto maana ajari za moto hatujui zitatokea kwa nani na wakati gani.

Mhe. Waziri Bashungwa amemalizia kwa kutoa mkono wa pole kwa wahanga wa ajali ya moto kiasi cha shilingi milioni moja laki mbili pia ametoa laki moja kama pongezi kwa askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Koplo Denis Minja aliyemuokoa mtoto kwenye shimo la choo siku tatu zilizopita.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka ametoa mapendekezo yatakayosaidia kukokomesha majanga ya moto wilayani Karagwe

“Wafanyabiashara waweke walinzi wenye uhakika maana walinzi wengi ni wazee sana na walevi, kila duka liwe na kifaa cha zima moto ili kusaidia kuzima milipuko kabla haijasambaa Zaidi, jeshi la polisi lisaidiane na walinzi wa kijamii katika ulinzi shirikishi ili kudhibiti uzurulaji wa vibaka usiku”

 

No comments :

Post a Comment