************************************
Kwa asiyejua
kilichojificha nyuma ya pazia yano #Demokrasia anaweza kudhani ni uwanja
sawa wa kisiasa unaowezesha watu kushiriki shughuli za kisiasa kupitia
vyama kushindanisha sera, hoja na Ilani za vyama vyao ili kuaminiwa,
kupigiwa kura na kuchaguliwa kwa viongozi kushika madaraka kwa njia ya
kidemokrasia.
Lakini ukweli ni
kwamba, duniani kuna mifumo miwili ambayo inashindana kila mfumo ukitaka
kuitawala dunia kupitia kunadi sera zake, ikiwemo kuwaweka madarakani
viongozi wenye kulinda maslahi ya mifumo hiyo. Mifumo hiyo ni Ubepari na
Ujamaa (Ukomunisti au Usoshalisti). Mfumo wa Ubepari asili yake ni nchi
za Magharibi na mfumo wa Ujamaa au Ukomunisti na Usoshalisti ni nchi za
Madhariki.
#UBEPARI: Huu ni
aina ya mfumo wa uchumi unaowawezesha kundi la watu wachache kuhodhi na
kumiliki njia kuu za uchumi huku kundi kubwa la watu likibakia masikini
na kutumikishwa kama vibarua na kundi la wachache. Kwenye mfumo huu,
kati ya rasilimali zinazomilikiwa na wachache ni pamoja na ardhi.
#UJAMAA: Huu ni
aina ya mfumo wa kiuchumi unaowezesha njia kuu za kiuchumi ikiwemo
ardhi, viwanda, mashirika ya uzalishaji mali, taasisi za fedha ikiwemo
mabenki kumilikiwa na umma kwa maslahi ya wengi, na faida inayopatikana
hugawanywa na kutumika kupitia huduma za kijamii kama vile afya, elimu,
maji, umeme na ujenzi wa miundombinu. Mfumo huu hutumika zaidi kwenye
nchi zenye kufuata sera ya haki sawa kwa wote ikiwemo Tanzania.
#UJIO_WA_DEMOKRASIA_NA_MALENGO_YAKE:
Huko nyuma mfumo
wa utawala uliofuata siasa za Ujamaa au Kikomunisti ulionekana kutokuwa
na utaratibu wa viongozi kuachia madaraka au kupokezana nafasi za juu za
uongozi baada ya mihula fulani kwa kiongozi kukaa madarakani. Kwa
msingi huo, sehemu kubwa ya viongozi walioshika madaraka hawakuweza
kuondoka kwa hiyari yao hadi kifo kitokee.
Kilichotokea ni
kwamba, kuwepo kwa mfumo wa Kijamaa au Kisoshalisti duniani kulizinyima
fursa nchi zenye kufuata mifumo ya kibepari kuweza kupata mwanya wa
kunyonya rasilimali za kiuchumi kutoka nchi za kijamaa na kikomunisti
ikiwemo madini na mali ghafi za viwandani.
Kwa msingi huo,
demokrasia ya mfumo wa vyama vingi iliyopo duniani kwa sasa ilibuniwa na
nchi za Magharibi kwa lengo la kufadhiri na kupandikiza viongozi
vibaraka madarakani kwenye nchi zenye rasilimali kupitia uchaguzi wa
kidemokrasia, huku lengo na madhumuni likiwa kurahisisha uchotwaji wa
rasilimali hizo kupitia viongozi walionunuliwa walioko madarakani.
Hii ni baada ya
kutambua kwamba, kupitia mfumo wa Kijamaa na Kikomunisti, isingewezekana
kupata viongozi vibaraka na pandikizi watakaoruhusu rasilimali za nchi
kunyonywa kurahisi.
#DEMOKRASIA_INAPOSHINDWA_NINI_HUFANYIKA?
Mfumo huu wa
mataifa makubwa yenye nguvu za kiuchumi duniani, kupandikiza viongozi
vibaraka madarakani kwa lengo la kuwatumia kunyonya rasilimali za
mataifa yao, umekuwepo kwa kipindi kirefu, ambapo katika baadhi ya nchi
umeshindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa kutokana na misimamo na
uzalendo wa viongozi na wananchi wa nchi husika, na hivyo mabeberu
wameanza kutumia mbinu nyingine mbadala, kama vile kufadhiri na
kuchochea wananchi kutotii sheria za nchi na kuhasi serikali za nchi zao
kwa kufanya maandamano, fujo, vurugu, uharibifu wa mali, ili nchi
isitawalike, na hali hiyo inapotokea, mataifa hayo huingilia kati kuunga
mkono wenye kuandamana kwa kisingizio cha kulinda demokrasia, uhuru wa
kujieleza pamoja na haki za binadamu.
Hicho ndicho
kilichotokea nchini Iraq, Libya, Tunisia, Syria, Misri, na sasa Iran na
Venezuela. Suala la demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza
ni agenda inayotumiwa na mataifa makubwa ili kufikia malengo yao.
Mbinu hii ya
kuwatumia viongozi vibaraka kuwapandikiza madarakani inaposhindwa kuzaa
matunda, hatua inagofuata ni kutafuta kisingizio cha kuiwekea vikwazo
vya kiuchumi nchi husika hadi pale itakaposalimu amri. Miongoni mwa nchi
zilizokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Zimbabwe, Cuba na Venezuela.
Hivyo ndivyo
Marekani na washirika wake nchi za Jumuiya ya Ulaya zinavyofanya dhidi
ya nchi zenye rasilimali kwa lengo la kujinufaisha na rasilimali za nchi
masikini ikiwemo Tanzania, ambapo Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Seif
Sharif Hamad ni kati ya vibaraka waliokwisha ingia kwenye rada za
mataifa hayo, na wako tayari kufanya lolote baya kwa nchi yao ili
kutimiza lengo lililokusudiwa ikiwemo kuunga mkono mapenzi ya jinsia
moja, wanafunzi wa kike kuruhusiwa kubeba mimba wakiwa bado shuleni.
Unapoona mataifa
ya Ulaya na Marekani yakiingilia mambo ya ndani ya mataifa mengine kwa
kisingizio cha kudumisha haki za binadsmu, demokrasia, na uhuru wa
kujieleza, hayafanyi hivyo kwa nchi masikini zisizo na rasilimali bali
yanaangaika na mataifa yenye rasilimali za kiuchumi kwa ajili ya mataifa
yao kama vile mafuta, madini na mali ghafi ya mazao kwa ajili ya uchumi
wa viwanda vyao.
#FUNDISHO_KWETU_WATANZANIA:
Pamoja na kwamba
ni hulka ya binadamu kutojifunza siku zote kutokana na makosa ya
mwenzake mpaka yamkute mwenyewe ni muhimu kwetu sisi watanzania
kujifunza na kuzibaini mbinu mbali mbali chafu zinazotumiwa na mabeberu
kupandikiza viongozi vibaraka mfano wa Tundu Lissu, Zitto Kabwe, na Seif
Sharif Hamad wanaotafuta madaraka ikibidi hata kwa njia ya kumwaga damu
ili wafikie malengo waliyotumwa na mabwana zao.
Tunachotakiwa
kufanya, licha ya kuwepo mfumo wa kisiasa wa kidemokrasia unaoruhusu
viongozi vibaraka kugombea kupitia vyama vya siasa vinavyofadhiriwa na
mabeberu, ni kutoruhusu viongozi wa aina hiyo kupata nafasi ya kuongoza
mataifa yetu.
Kamwe tusiruhusu
wala kukubali kiongozi kibaraka mwenye kushirikiana na mabeberu, iwe
kupitia siasa au harakati za kijamii, kwa malengo hasi kwa nchi yetu
kujiinua na kustawi ka walivyojiinua Jonas Savimbi wa Angola, Rieck
Machar wa Sudan kusini na wengineo.
Amani, utulivu, umoja na mshikamano wetu ni muhimu zaidi kuliko maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.
No comments :
Post a Comment