Tuesday, November 3, 2020

NATIRO WAHITAJI MSAADA ,CRDB YAANZISHA MWENDO KWA MIL 10


Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Benki ya CRDB ,Siaophoro Kishimbo akizungumza wakati wa mahafali ya 34 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Natiro iliyopo wilaya ya Moshi alipokuwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 34 ya wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Natiro,Siaophoro Kishimbo ambaye pia amewahi kusoma katika shule hiyo iliyopo wilaya ya Moshi akitoa nasaha kwa wahitimu hao.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza wakati wa mahafali ya 34 ya wahitimu katika shule ya sekondari ya Natiro iliyopo wilaya ya Moshi .
Baadhi ya Mameneja wa matawi ya Benki ya CRDB yaliyopo mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika sherehe ya mahafali ya 34 katika shule ya sekondari ya Natiro.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Natiro Mchungaji Yudah John Lenare akizungumza kwa niaba ya Bodi wakati wa mahafali ya 34 ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule hiyo.
Baadhi ya Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu katika shule ya sekondari ya Natiro wakionekana na sura za furaha wakati wa sherehe ya mahafali ya 34 ya wanafunzi hao.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Natiro Emanuel Mrema akitoa taarifa ya shule kwa wageni waliofika katika mahafali ya 34 ya shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne wakiimba nyimbo wakati wa sherehe ya kuagwa iliyofanyika katika shule ya sekondari ya Natiro iliyopo wilaya ya Moshi 
Mameneja wa Matawi ya Benki ya CRDB mkoa wa Kilimanjaro wanawake wakiongozwa na Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa (kushoto) wakati wakitamburishwa kwa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Natiro.
Mameneja wa Matawi ya Benki ya CRDB mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamebeba zawadi maalumu kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki ya CRDB ,Siaophoro Kishimbo akikabidhi zawadi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Natiro waliofanya vizuri katika mitihani yao.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 34 ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Natiro ,Siaophoro Kishimbo akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa shule hiyo pamoja na mameneja wa matawi ya CRDB Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa sherehe za mahafali hayo..
Mgeni rasmi katika mahafali ya 34 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Natiro akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa shule hiyo pamoja na wahitimu .Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro 

SHULE ya Sekondari ya Natiro iliyopo wilaya ya Moshi mkoani inahitaji kiasi

cha Sh Mil 100 ili kupunguza changamoto zinazoikabili ikiwemo umaliziaji wa jengo la Bweni kwa ajili ya wasichana ,ujenzi wa Choo cha Wavulana, ujenzi wa Bwalo na maktaba .

Mkuu wa shule hiyo Emanueli Mrema aliyasema hayo wakati wa mahafali ya 34 ya shule yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo kijiji cha Natiro Kilometa 14 kutoka Moshi mjini ikiwa na idadi ya wanafunzi 231 kati yao wavulana wakiwa ni 116 na wasichana wakiwa 157.

“Licha ya mafanikio tuliyonayo bado tunakabiliwa na changamoto ambazo ni pamoja na miundombinu isiyokidhi mahitaji ya shule ikiwemo Bweni la wasichana,Choo cha Wavulana  na jengo la maktaba pamoja na maeneo mengine ya shule ambayo ni chakavu”alisema Mrema.

“Ushiriki wa wadau wa elimu katika mahafala haya ni sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazoikabili shule yetu kwani ili kukabiliana na kupunguza makali ya changamoto hizo tunauhitaji wa kiasi cha sh Mil 98.3”aliongeza Mwl Mrema.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye pia ni mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari Natiro miaka 20 iliyopita,Mkurugenzi wa rasilimali watu Benki ya CRDB, Siaophoro Kishimbo akajibu sehemu ya changamoto hizo katika hotuba yake.

“Najua shule inachangamoto nyingi sana ambazo zote tungependa ziweze kutatuliwa na sisi tunaamini kwamba huu ni mwanzo tu wa mashirkiano mazuri ambayo benki yetu itakuwa nayo na shule hii na kwa kuanzia katika ile gharama y ash Mil 98 sisi kama benki tutatoa sh Mil 10.”alisema Kishimbo

“Tunaamini kwamba hizi fedha hazitoshi lakini ni kiwango ambacho kinaweza kikasaidia shule kuweza kuimarisha miundombinu yake ili vijana wanaokuja hapa waweze kusoma kwa utulivu na waweze kufaulu kwa viwango vya ju.” Aliongeza Kishimbo .

Akitoa nasaha kwa vijana hao Kishimbo aliwataka wahitimu hao kutopoteza muda mwingi wawapo katka maneo ya shule kwani wazazi wamekuwa wakihangaika kutafuta adaili wao waweze kusoma bila ya changamoto ya kurejeshwa majumbani kwa ajli ya kukosa ada

“Kuna msemo unasema jiandae vizuri kabla ya vita ili wakati wa vita ukifika usiwe ni wakati wa wewe kujifunza mbinu mpya bali kuchagua ni silaha gani ya kutumia ,usipoteze muda mwingi unapokuwa maeneo haya wazazi wanalipa ada kwa uchungu sana na wengine pengine tunarudishwa ada mara nyingi hatuna ,ukipata nafasi itumie nafasi ipasavyo ,muda wa kucheza haupo”alisema Kishimbo.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa aliwashauri wahitimu hao kuanza kutengeneza na kushikilia ndoto zao ili kufikia malengo ya nani wanataka kuwa ikiwa ni pamoja na kundoa matamanio ya ujana ambayo yanaweza kufifisha ndoto zao.

Mgeni rasmi amekabidhi vyeti kwa Wahitimu huku Benki ya CRDB ikitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ikiwa ni pamoja na kufunguliwa akaunti.

No comments :

Post a Comment