Mkurugenzi
wa Utafiti na Huduma za Uuguzi na Oparesheni wa Hospitali ya Shree
Hindu Mandal Kishan Mistry akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana
na huduma wanazozitoa za upimaji na ushauri bure katika wiki ya
Maadhimisho ya Magonjwa Yasiyoyakuambukiza jijini Dar es Salaam.
Mmoja
ya mwananchi akipata huduma ya macho katika hospital ya Shree Hindu
Mandal katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa Yasiyoyakuambukiza.
Mkazi
wa Gongolamboto Philmont Matiko akizungumza namna alivyopata huduma
katika Hospital ya Shree Hindu Mandal katika Maadhimisho ya Magonjwa
Yasiyoyakuambukiza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma na ushauri bure katika hospitali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
HOSPITALI
ya Shree Hindu Mandal imesema katika kuadhimisha Wiki ya kuzuia na
kudhibiti magonjwa yasiyoyakumbukiza watatoa huduma za bure za kupima na
kutoa ushauri kwa wananchi wataokwenda katika hospitali
hiyo.
Huduma
wanazozitoa katika maadhimisho kwa vipimo na ushauri ni magonjwa ya
Kisukari, Kansa, Shinikizo la damu (BP) na huduma za macho ambapo
katika magonjwa hayo yapo mengine ni ushauri na kubadili mfumo wa
kuishi baada ya kuonekana na viashiria vya ugonjwa.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho hayo kwa niaba Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali
ya Shree Hindu Mandal Mkurugenzi wa Utafiti za Huduma za Uuguzi na
Oparesheni Kishan Mistry amesema katika maadhimisho hayo Manispaa ya
Ilala ndio imeipa jukumu hospitali hiyo kutoa huduma za kupima magonjwa
mbalimbali kwa siku tatu mfululizo na kuungana na serikali siku ya
Alhamis hadi Jumamosi kwa kutoa huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Mistry
amesema kuwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi
katika hospitali hiyo kupata vipimo pamoja na ushauri katika magonjwa
yasiyoyakuambikiza kwani wakati mwingine mtu anaweza kuhisi mzima kumbe
ana tatizo ambalo likiibuka linakuwa ni shida.
Muuguzi
wa Mshauri wa Ugonjwa wa Kisukari wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal
Mary Nghumbu amesema kuwa ugonjwa wa kisukari kina mambo mawili moja ni
kurithi na pili mfumo wa maisha unaotokana ulaji uliopitiliza kwa
mahitaji ya mwili usiozingatia lishe.
Amesema
kuwa katika kuepukana na tishio la ugonjwa wa kisukuri pamoja na
shinikizo la damu njia rahisi ni kufanya mazoezi mara kwa mara kuepukana
na vyakula vya mafuta yaliyokupitilizta na kuzingatia ulaji unafuata
lishe kwa kuzingatia mpangilio wa chakula.
Mkazi
wa Gongolamboto Philimon Matiko amesema utaratibu wa Hospitali hiyo
kutoa huduma na vipimo ni suala la kujenga uimara kwa afya za watanzania
na kushauri kufika vijijini.
No comments :
Post a Comment