HIFADHI za taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika bara ya Afrika kwa mwaka 2020.
Katika taarifa iliyotolewa na Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi-
Mawasiliano, Pascal Sheltete, imesema tuzo hizo zimetangazwa jana Novemba 9, 2020 na taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya Mtandao.ITaarifa hiyo imesema kuwa hii ni mara ya pili kwa hifadhi ya taifa ya Serengeti kushinda katika kundi la hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi bara la Afrika.
"Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za central kalahari ya Botswana, Etosha ya Namibia, Kidepo Valley ya Uganda Kruge ya Afrika Kusini na Masai Mara National Reserve ya Kenya."
Imeeleza kuwa Serengeti inajivunia umaarufu wa Msafara wa Nyumbu uhamao zaidi ya milioni Moja na nusu,aina mbalimbali za wanyama pori wanaopatikana kwa wingi, maadhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimbali za utalii zinazovutia watalii wengi.
Aidha
TANAPA imeishukuru serikali, wananchi, wadau wa utalii pamoja na watu
wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya serengeti kuwa mshindi
wa hifadhi boara zaidi kwa bara la Afrika 2020.
No comments :
Post a Comment