Tuesday, November 17, 2020

WAZAZI WATAKIWA KUWA WALINZI WA WATOTO.


Bi. Asia Mkene Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala akitoa huduma kwa mwananchi aliyefika kwenye la hospitali hiyo kwenye maonesho ya maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza kwenye viwanja vya mnazi mmoja yaliyofanyika jijini Dar es Salaam,kulia ni Koplo Salome Izina

***************************************

Na. Catherine Sungura, WAMJW-Dar es Salaam

Wazazi wametakiwa kuwa walinzi wa watoto ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Rai hiyo imetolewa na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Musa Maroko wakati wa maonesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyomalizika mwishoni mwa wiki viwanja vya mnazi mmoja jijini hapa.

Maroko alisema kuwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukatili kwa watoto bado vinaongezeka miongoni mwa jamii kila siku.

“Kutokana na hali hiyo hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala imeanzisha huduma jumuishi kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hususan wakati wa Kinondoni, Ubungo na Dar es Salaam kwa ujumla”.

Alifafanua kuwa lengo la kuanzisha huduma hiyo ni kuwasaida wananchi ambao hawawezi kwenda polisi hivyo kituo hicho kinawasaisia kupata huduma nne kwa pamoja ikiwemo ya kisheria,kitabibu,kipolisi na ustawi.

“Mtu anapopata tatizo la kingono anapaswa kutopoteza ushahidi ili kuweza kuwa rahiai kushughulikia tatizo hilo,kwahiyo akifika ataonwa na ushahidi utawekwa kwa kufuata taratibu zote za kisheria na kuhifadhiwa kwa usalama”.

Naye Koplo Salome Izina kutoka kituo hicho alisema huduma hiyo imekuwa na mafanikio kwenye kanda yao kwani inampunguzia gharama mwananchi na kuweza kupata vielelezo vilivyo sahii kutoka maabara kwenye hospitali hiyo.

Hata hivyo Koplo Izina aliwataka wazazi kutochelewa kutoa taarifa mara baada ya kujua tatizo limetokea ili kupata ushahidi mzito wa kuweza kumuunganisha na mtuhumiwa.

Wakati huohuo Afisa Ustawi wa Jamii wa hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Bi. Asia Mkene alisema bado wanawake wengi wananyamaza wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia na sababu kubwa ni kutokuwa na elimu ya kutosha na hivyo hushindwa kuripoti.

Alisema kituoni hapo asilimia 87 za kesi wanazopokea ni za watoto ikifuatia wanawake ila bado kesi za akina
baba ni asilimia ndogo.

 

No comments :

Post a Comment