Wadau
wa Maendeleo jiji la Arusha wakiwa katika kikao Kazi kilichoandaliwa na
Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha, Mgeni Rasmi alikuwa Afisa
Maendeleo Mkoa Blandina Nkini hayupo pichani, Wadau hao wamebariki wiki
ya kisheria kufanyika na kudai watashiriki kwa pamoja.
(Picha na Woinde Shizza, ARUSHA)
Na Woinde shizza , ARUSHA
WATOA
huduma wa msaada wa kisheria mkoa wa Arusha wamejipanga kutumia
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria kwa kuwatembelea maabusu
waliopo kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria.
Hayo
yalisemwa na afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha ambae pia ni
msajili msaidizi wa watoa huduma wa msaada wa kisheria mkoa wa Arusha
Blandina Nkini wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana na maandalizi
ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria kwa mkoa wa Arusha
yanayotarajiwa kuanza nchi nzima Novemba 12 Hadi 18.
Alisema
kuwa kufuatia maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoa wa Arusha
kwa kushirikiana na jiji la Arusha wamefanya maandalizi ya maadhimisho
hayo ambapo wanasheria wamejipanga kutembelea mahabusu ili kuwapatia
msaada wa kisheria pamoja na kuweka kituo cha kutoa huduma katika kata
ya muriet.
"Tutatembelea
mahabusu zote za watoto pamoja na watu wazima ili kuenda kusikiliza
kesi mbalimbali zinazowakabili, ambapo tutawapa msaada wa kisheria mara
baada ya kuzisikiliza ambapo pia katika wiki hiyo tutaeka kituo katika
kata ya Muriet." Amesema Nkini
Aidha
Nkini alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika wiki hiyo ya
kisheria ,ili kuweza kupata msaada wa kisheria kwani wanasheria
watakuwa tayari kuwasikiliza na kuwasaidia,huku alibainisha kuwa huduma
hiyo wataitoa bure katika wiki hiyo ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa
kisheria.
No comments :
Post a Comment