Na Mwandishi Wetu
BODI
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya
wanafunzi 5168 wa awamu ya pili wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo
yenye thamani ya TZS 19.9 bilioni.
Taarifa
iliyotolewa katika vyombo vya habari na Mkurugenz Mtendaji wa HESLB,
Abdul-Razaq Badru inasema hadi leo (Jumanne, Novemba 17, 2020), jumla ya
wanafunzi 52,473 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mkopo yenye thamani ya
TZS 170.02 bilioni.
Basru
alisema Novemba 11, mwaka huu HESLB ilitangaza orodha ya Awamu ya
Kwanza waliopangwa mikopo iliyokuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza
wapatao 47,305 ambao walipangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 150.03
bilioni.
“Wanachotakiwa
kufanya kwa sasa ni kutembelea katika akaunti zao za SIPA walizotumia
kuomba mkopo na watapata taarifa za kina kuhusu mkopo.” amesema
Abdul-Razaq Badru leo (Jumanne, Novemba 17, 2020) Jijini Dar es Salaam.
Waliokosea sasa ruksa kurekebisha
Kuhusu
wanafunzi waombaji ambao maombi yao yalikua na upungufu, Badru amesema
HESLB imetoa muda wa siku tano (05) kuanzia kesho (Jumatano, Novemba 18,
2020) kurekebisha taarifa zao na kuzituma kwa njia ya mtandao.
“Tuna
wanafunzi wachache ambao maombi yao yana upungufu ambao kuanzia kesho
wataweza kuingia katika akaunti zao za SIPA walizotumia kuomba mkopo na
kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi na tutazifanyia uchambuzi na wenye
sifa watapangiwa mikopo mapema iwezekanavyo,” amesema Badru.
katika
mwaka 2020/2021, Serikali imetenga kiasi cha TZS 464 Bilioni kwa ajili
ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu 145,000 wakiwemo
wanafunzi 54,000 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 91,000 wanaoendelea na
masomo.
No comments :
Post a Comment