Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James akitoa mada
kuhusu namna ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu
janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda
namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu leo
kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waandishi wa habari nchini
na wananchi wameombwa kutumia mfumo wa kidigitali wa kutoa taarifa za
matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu uitwao “Haki
Kiganjani” wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa
kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486.
Wito huo umetolewa na Afisa
TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights
Centre – LHRC), Nikumwitika James wakati mafunzo ya Sheria za Uhuru wa
Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa (Shinyanga, Mwanza, Geita,
Kagera na Mara) ili kuwajengea uwezo kuzielewa sheria zinazoongoza
Tasnia ya Habari nchini.
Nikumwitika amewashauri
waandishi wa habari kutumia mfuko mfumo wa kidigitali kutoa taarifa za
matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu wanayokutana nayo lakini pia
watoe elimu kwa wananchi Jinsi ya kutumia Application ya ‘Haki
Kiganjani’ kwa kutumia simu janja au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe
mfupi SMS) kwenda namba 0699695486.
“Watu wana matatizo lakini
hawajui wayapeleke wapi, wayaripoti wapi. Naomba mtusaidie kuwapa namba
hii ya simu 0699695486 ya simu watume sms/ujumbe au muwafahamishe
kupakua/Ku – download App ya ‘Haki Kiganjani’ iliyopo Playstore ambayo
itawezesha kutuma taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za
binadamu”,amesema.
Afisa Programu wa LHRC
Wakili Fortunata Ntwale amesema mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha
waandishi wa habari kuzijua sheria zinazohusu tasnia ya habari ili
waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.
“Lengo la LHRC imetoa
mafunzo haya katika Kanda saba nchini na kwa muda wa siku mbili tumetoa
kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa ili kuboresha uhuru wa habari na
uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari”,amesema.
“Kutokana na utungwaji na
mabadiliko mbalimbali ya sheria za wanahabari LHRC imewajengea uwezo
waandishi wa habari juu ya sheria mbalimbali zinazoongoza tasnia ya
habari ili kupunguza changamoto zitokanazo na ukiukwaji wa sheria kwa
waandishi wa habari”,ameongeza Ntwale.
Amesema mbali na kuwajengea
uwezo waandishi wa habari katika sheria za uhuru wa kujieleza pia
wametoa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa kidigitali wa kutoa
taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ujulikanao kama
‘Haki Kiganjani’.
Afisa TEHAMA wa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC),
Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya
‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida
kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya
ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya
Ziwa. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Afisa TEHAMA wa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC),
Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya
‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida
kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya
ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.

‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ kuripoti matukio ya

Wakili wa Kujitegemea Pasience Mlowe akitoa ufafanuzi kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Wakili wa Kujitegemea Pasience Mlowe akitoa ufafanuzi kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akiwasihi waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia sheria.
Afisa Programu wa LHRC
Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Kushoto ni Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal
and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James.
Mwandishi wa habari Rose
Mweko kutoka mkoa wa Geita akitoa neno la shukrani kwa LHRC kwa niaba ya
washiriki wa mafunzo hayo kutoka mkoa wa Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara
na Kagera kutoa mafunzo ya sheria zinazohusu tasnia ya habari.
Washiriki wa mafunzo hayo wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo ya siku mbili.
Washiriki wa mafunzo hayo wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo ya siku mbili.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment