Thursday, November 19, 2020

WAJUE MAWAZIRI WA SERIKALI YA AWAMU YA NANE ZANZIBAR

WAJUE MAWAZIRI WA SERIKALI YA AWAMU YA NANE ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi Leo ametangaza Baraza jipya la Mawaziri ambao wataongoza jkatika Serikali ya awamu ya nane hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja.

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji – Mh. Mudrik Ramadhan Soraga.

2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Masoud Ali Mohammed.

3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora Mh. Haroun Ali Suleiman.

4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mh. Jamal Kassim Ali.

5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mh. Dk Khalid Mohammed Salum.

6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo Mh. Soud Nahodha Hassan.

7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Simai Mohammed Said

8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni Mh. Tabia Mwita Maulid.

9. Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri.

10. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi – Bi Riziki Pembe Juma.

11. Wizara ya Maji na Nishati Suleiman Masoud Makame.

12. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Hakuna Waziri.

13. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Bi Lela Mohammed Mussa.

14. Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi Mh Abdallah Hussein Kombo.

15. Wizara ya Ujenzi Bi Rahma Kassim Ali.

DK. HUSSEIN:NITAEKA MANAIBU WAZIRI KAMA WATAHITAJIKA

 “Nimetangaza Mawaziri pekee leo, Manaibu Waziri nitawaweka wakihitajika, nakusudia kupunguza idadi ya Watu Serikalini, penye mahitaji tutaweka, Wizara kubwa sana kazi ni nyingi sana tutawaweka ila sehemu nyingi hatutoweka ili kupunguza idadi”-Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi 

“Kuhusu Idadi ndogo ya Wanawake kwenye Baraza, mimi ni Muumini wa kutoa nafasi kwa Wanawake ila unapofanya uteuzi unaangala sifa sio jinsia, bado tupo kwenye uuandaji wa Serikali kukiwa na nafasi na wapo wanaostahili tutawapa, ila lini tutafika 50 kwa 50 sio rahisi kusema” Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi 


“Moja ya kazi nitakazowatuma Mawaziri ni kuhakikisha wanakusanya kodi kwa wingi, mengi nitawaambia siku ya kuwaapisha, kuhusu michezo nipo tayari kukaa na wadau wa michezo tuangalie kila ambalo ni la kujenga kwenye michezo tulifanye kazi ili kuiinua” Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi 

 

No comments :

Post a Comment