Wednesday, November 11, 2020

Vodacom yazindua huduma ya duka jongefu, inakuletea huduma mlangoni kwako

Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa (katikati), Mkuu wa mauzo na usambazaji George Lugata na Msimamizi wa Duka, Emmanuel Makaki wakikata utepe kuzindua huduma ya duka jipya la Vodacom linalotembea (Vodacom Mobile Shop) ambao litawezesha wateja kupata huduma popote walipo. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika leo Kariakoo jijini Dar es Salaaam
Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa akipunga mikono kuashiria uzinduzi wa huduma ya duka jipya  la Vodacom linalotembea (Vodacom Mobile Shop)

 Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania Plc leo imezindua huduma mpya, ya kwanza kwenye soko la tasnia ya mawasiliano – Huduma ya duka jongefu inayolenga kupeleka huduma kwa wateja popote walipo.

Huduma hii ya duka jongefu ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika tasnia ya mawasiliano itanufaisha wateja wa Vodacom ambao wanahitaji huduma ya haraka na inayofaa popote. Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi katika Soko la Kariakoo, Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Vodacom, Linda Riwa alisema huduma mpya ya duka jongefu ni mfano wa kuigwa inayopeleka huduma kwa wateja katika maeneo waliyopo.

"Tunaposherehekea miaka 20 ya kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia utoaji wa bidhaa na huduma za kipekee kwenye Mtandao wetu Supa, tunatambua kuwa wateja wetu ndio sababu ya sisi kuwepo sokoni, hivyo tumeadhimia kuwapa huduma bora kadri inavyowezekana. Kwa hiyo leo Vodacom tunazindua duka la kwanza la aina yake ambalo litaleta huduma zote ambazo zinaweza kupatikana katika duka lolote la Vodacom milangoni kwa wateja wetu,” alisema Linda.

Vodacom ikiwa na zaidi ya maduka (Vodashops) 100 pamoja na madawati ya Huduma (Service desks) 439, inajivunia kwa kuwa mtandao mkubwa na wenye nguvu katika tasnia ya mawasiliano. Pamoja na kuongezewa huduma ya duka la simu jongefu ambayo itapatikana katika eneo jipya kila siku, wateja wa Vodacom watapata huduma kwa karibu zaidi. Huduma hii inaanzia Jijini Dar es salaam kisha itaendelea katika mikoa yote nchini.

"Tunakwenda mbali zaidi, sio tu kwa kutoa huduma zetu kwenye simu za wateja kupitia zana (Apps) bora za kidijitali kwa kutoa mipango mbalimbali  kama ya MyVodacom na M-Pesa, lakini sasa tunaboresha utoaji wetu wa huduma kwa wateja kwa kuhakikisha tunapatikana mahali popote walipo kama vile  mahali pao pa kazi, sehemu za biashara au sehemu za makazi na kwa urahisi zaidi, ” aliongeza Linda.

Duka jongefu litatoa huduma nyingi kama vile kujibu maswali ya wateja, usajili wa laini kupitia alama za vidole (biometric registration), uuzaji wa simu za aina mbalimbali pamoja na vifaa vyake na bidhaa zingine za maisha ya kidijitali na huduma kama vile M-Pesa n.k.

“Kwa hiyo wakati wa msimu huu wa sikukuu, angalia huduma ya duka la simu jongefu jirani na eneo ulilopo ili upate bidhaa na huduma mbalimbali  zinazoletwa katika eneo lako kwa urahisi wa maisha na kuokoa muda ambao ungeenda kufuata huduma hiyo,” Linda alihitimisha.

 

No comments :

Post a Comment