Mkuu
wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (kulia) na Mkurugenzi wa Uhusiano
na Mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Rosalynn Mworia wakikata utepe
kuzindua duka la kwanza la kampuni hiyo lililopo mjini Kisarawe, duka
hilo litatoa huduma zote kwa wateja wa Vodacom.
Mheshimiwa Jokate Mwegelo akicheza ngoma ya asili kushrehekea kuzinduliwa kwa duka hilo jipya
Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo jirani na stendi ya Kisarawe
Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya Pwani akiwakaribisha wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka hilo.
Mkuu
wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akimkabidhi zawadi ya simu mteja
wa muda mrefu wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc
Saleh Semjaila, sanjari na uzinduzi wa duka la kwanza la kampuni hiyo
lililopo mjini Kisarawe, katikati ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo,
Mwanana Shabani.
No comments :
Post a Comment