Tuesday, November 10, 2020

Vodacom Tanzania PLC na Laina Finance Waingia Ubia, Kuleta Simujanja (Smartphones) Kwa Watanzania

Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, George Lugata (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mkopo wa simujanja itakayowezesha wateja wa Vodacom Tanzania kukopeshwa  simu katika maduka ya kampuni hiyo yaliyoenea kote nchini. Kulia ni Meneja Mkuu wa Laina Finance Limited, Mrisho Shomari ambao ni wabia wa huduma hii.

…………………………………………………………………………

 Dar es salaam.

Katika harakati za kushinikiza upenyaji wa simujanja nchini, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC imeingia ubia na Laina Finance Limited kuleta mpango mpya wa ufadhili wa simujanja  unaowezesha Watanzania wengi zaidi  kupata simu bora na za kisasa kwa njia rahisi na nafuu zaidi.

Taarifa za mara kwa mara kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) zinaonyesha ukuaji

thabiti wa matumizi ya simujanja pamoja na matumizi ya tovuti nchini, ambapo matumizi ya intaneti yamefikia kiwango cha asilimia 48. Licha ya ukuaji huu, inakadiriwa kuwa theluthi mbili kati ya tano ya idadi ya watu nchini hubaki nje ya mtandao na wametengwa na faida za kijamii na kiuchumi zinazoletwa na matumizi ya  intaneti. 

Kupunguza mgawanyiko huu wa kidijitali ni muhimu ili kuchochea malengo ya Tanzania, ya kubadilisha kutoka uchumi wa kilimo wa muda mrefu  hadi kuwa uchumi wa maarifa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Upatikanaji wa  simujanja kwa bei nafuu ndio ufunguo wa kuziba pengo hili na kuhakikisha kila Mtanzania ameunganishwa kwenye mtandao. Ushirikiano wetu na Vodacom Tanzania PLC – kampuni ya simu inayoongoza kidijitali nchini – tutatumia uzoefu wetu katika huduma za kifedha na utaalam katika teknolojia kusaidia wateja wao kote nchini kupata simu za bei nafuu kupitia mikopo rahisi,” alisema Meneja Mkuu wa Laina Finance Limited, Mrisho Shomari.

Wateja wa Vodacom Tanzania PLC wanaweza kuomba mkopo wa simujanja  katika maduka ya kampuni ya Vodacom Tanzania PLC yaliyoenea kote nchini kwa mkopo, baada ya kufanyiwa tathmini. Pamoja na mpango wa ufadhili, wateja wanaweza kupata simujanja yenye thamani ya hadi shilingi milioni moja  baada ya amana ya awali ya asilimia 40  ikifuatiwa na awamu rahisi za marejesho kila mwezi za hadi miezi 3,  kupitia M-Pesa.

“Kukuza ujumuishwaji wa kidijitali kunamaanisha kila Mtanzania anapata simujanja  na kama kampuni tumeandaa mikakati tofauti ili kuhakikisha simujanja zinaenea nchini pamoja na kusambaza simu bora na za bei rahisi kama vile smartkitochi ambayo inauzwa kwa shilingi  48,000 na sasa zinapatikana kupitia huduma hii ya kifedha,” alisema Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, George Lugata.

Ili kupata mpango huu wa ufadhili, mteja anapaswa kukubali taarifa zake za matumizi ya GSM zitumike na kampuni ya Laina ili kufanya tathmini ya mkopo, hii ni pamoja na kikomo cha kiwango cha juu cha ufadhili. Baada ya hilo, mteja basi atapokea ujumbe mfupi utakaomuongoza katika duka ambalo atakwenda kuchukua simujanja aliyochagua.

Kuhusu Vodacom:

Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza na wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa zaidi ya wateja milioni 15.5. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.

 

No comments :

Post a Comment