Kaimu MKurugrnzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
akizungumza mapema leo kuhusu shughuli za Ofisi hiyo pamoja na ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji unaoendela Mkoani Iringa. |
Bi Mary Mwangisa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu toka Tume ya
Taifa ya Umwagailiaji akizungumza kuhusiana na ushirikishwaji wa watumishi
wa kada mbalimbali katika mpango wa elimu kwa wakulima unaondelea
katika baadhi ya mikoa
Bw. Reginald Diamett Meneja Mfuko wa Maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji
toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongea kuhusu shughuli za mfuko
huo.
Tume ya Taifa ya umwagiliaji inaendelea na shughuli za maboresho ya miondombinu inayopeleka
maji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji za Ruaha Mbuyuni, Namagozi na Mlenge Pawaga MkoaniI ringa,iliyoharibiwa na mafuriko katika msimu wa mvua zilizopita.Hayo yameelezwa mapema leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiaji Bw. Daudi Kaali ambapo amesema katika skimu ya Ruaha Mbuyuni kazi ya kuchimba nakupanga mawe katika njia mpya yenye urefu wa mita 600 inakaribia kukamilika halikadhalika katika skimu za pawaga njia mpya yenye urefu wa mita 800 inachimbwa.
“Asimia (60%) yaukarabati wa miundombinu imekamilika katika skimu hizo, hivyo tunategemea mpaka mwishoni mwa wiki hii kazi itakuwa imekwisha kabisa.” Alisema Kaali
Akizungumzia Mradi wa Regrow unaosimamiwa na Wizara ya Maliasili na kutekelezwa na sekta husika Bw. Kaali alisema kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina kazi ya kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji ili kuweza kuleta ufanisi mkubwa wa matumizi sahihi ya maji iliyaweze pia kutumika katika hifadhi za taifa za ukanda wa kusini pamoja na shughuli nyingine za miradi ya maendeleo.
“Tume ina jukumu la kujenga Mfereji mkubwa wa maji wenye urefu wa kilometa tatu, kazi ambayo imefikia hatua yakutafuta mkandarasi kwa ajili ya ujenzi huo katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya madibila na unategemea kuanza mwezi ujao.” Alifafanua.
Akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiaji pamoja na mambo mengine unasimamia pia shughuli za maboresho ya miundombinu ya kilimo hicho.
Meneja wa Mfuko huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Reginald Diamett alisema lengo lingine la mfuko pia ni kujenga uelewa kwa wakulima na kuhamasisha tozo na makusanyo ya ada za hudu ma za umwagiliaji, jambo ambalo litaleta matarajio makubwa ya makusanyo katika sekta ya Umwagiliaji.
“Matarajio ni kwamba katika hekta zaidi ya laki sita zinazo mwagiliwa kwa sasa, katika msimu wa mavuno unaokuja, zaidi ya shilingi Bilioni hamsini na mbili (Bilioni 52) zinaweza kukusanywa ambapo Asilimia 75 (75%) itabakia kwa wakulima na asilimia ishirini na tano (25%) ndiyo itakayochangiwa katika mfuko wa umwagiliaji kama ada ya huduma ya umwagiliji.” Alibanisha.
Akizungumza kuhusu ushiriki wa kada mbalimbali za watumishi wa Tume katika kipengele cha kutoa elimu kwa wakulima Mkurugenzi wa Utawala na Rasimaliwatu Bi. Mary Mwangisa amesema kuwa hili linachangia kuwajengea uwezo wafanyakazi wa ndani kuhusu shughuli za Tume kuwa na uelewa pamoja na kuboresha kada mbali mbali katika sekta ya umwagiliaji Jambo ambalo pia limepelekea kupanua sekta hiyo kwa kuwapeleka watalam wa umwagiliaji katika ngazi za mikoa na wilaya.
Kwalengo la kusogeza huduma ya umwagiliaji karibu zaidi na wakulima ambao wengi zaidi wapo katika maeneo ya vijijini.
No comments :
Post a Comment