Picha ya msanii LULU ikionesha namna mwonekano wa picha ya mshindi wa Camon16 Billboard Star itakavyokaa kwenye bango
Akizungumza wakati wa kuitambulisha kampeni hiyo jijini Dar
es Salaam, meneja masoko mtandaoni Bi. Salma Shafi amesema wameandaa
kampeni hiyo maalum kwaajili ya wateja na wafuasi wao wa kwenye kurasa
zao mtandaoni.
“Hii ni kampeni ambayo inamtaka mshiriki kupiga picha yoyote
kwa ubunifu yaani ‘creative photo’ picha inaweza kuwa ya mtu au kitu
yenye ubunifu kwa kutumia TECNO CAMON 16 au simu yoyote ya toleo la
TECNO CAMON na ahakikishe ameweka water mark ili kutambulisha picha
imepigwa kwa simu ya toleo la TECNO CAMON. Akishapiga picha anatakiwa
aposti kwenye akaunti yake ya Instagram kwa hashtag
#Camon16BillboardStar” amesema Bi. Salma
Picha ya mtangazaji Omary Tambwe ikionesha namna mwonekano wa picha ya
mshindi wa Camon16 Billboard Star itakavyokaa kwenye bango
Bi. Salma ameongeza kuwa Kupitia kampeni hiyo ya ‘Camon 16
billboard star’ ambayo itadumu kwa muda wa wiki moja na mwishowe
watachaguliwa washindi watano na kuwa reposted kwenye ukurasa wa
Instagram ‘tecnomobiletanzania’ kisha kufanyiwa mchujo kwaajili ya
kupata mshindi mmoja.
Picha ya miss University Jihan Dimack Ikionesha namna picha ya mshindi wa itakavyokaa kwenye bango
Kampeni hiyo ya Camon16 Billboard Star, itafuatana na ziara
ya Camon16 ambapo washindi watapata nafasi ya kutembelea maeneo
mbalimbali ya hifadhi za Taifa ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro.
Je,
ungependa kufahamu zaidi kuhusu promosheni hii? Tafadhali tembelea
ukurasa wa TECNO Instagram kwa kubofya link hii;
https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/
No comments :
Post a Comment