Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) alipokuwa anawasili kwenye
kikao cha wafanyakazi jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akiongea na watumishi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa Waziri
Prof. Kabudi na Watumishi wa Wizara ulifanyika Jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge Ilani ya CCM na
nyaraka nyingine za utendaji Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb)akimkabidhi nyaraka Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora
Balozi, Anisa Mbega
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi
(Mb)akimkabidhi nyaraka Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Bibi.
Caroline Chipeta Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb)akiongea na Watumishi wa wizara katika mkutano
uliofanyika jijini Dodoma.
************************************
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
amesema Tanzania itashirikiana na nchi yoyote duniani ambayo inatambua
na kuheshimu Uhuru wa nchi na utu wa watu wake.
Prof. Kabudi ametoa kauli hiyo
jijini Dodoma alipozungumza na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi zake tangu alipoteuliwa na
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
“Tutafanya kazi na nchi zote
ambazo zinatuheshimu, zinatutambua kama Taifa huru, kutuheshimu sisi
kama binadamu wa mataifa mengine, hatutakubali kudharauliwa,
kutokuheshimiwa utu wetu na kudharauliwa kwa sababu ya misaada au pesa’,
amesema Prof. Kabudi
Ameongeza kuwa Tanzania
itasikiliza taifa lolote duniani na kujadiliana nalo kwa heshima kwani
mapungufu hayapo upande mmoja tu.
“Tuko tayari kuwasikiliza na
kujadiliana nao kwa heshima na kama wanadhani kuna kitu kimepungua kwetu
na sisi tunadhani kimepungua kwao,” amesema Prof. Kabudi.
Amesema Tanzania haiwezi kumruhusu mtu yeyote atumie misaada ya fedha kuondoa uhuru wetu na kutokuthamini utu wetu.
Amesema Tanzania haiwezi
kujitenga kama kisiwa na itaendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali
za kidunia kama vile kulinda amani, kukabiliana na mabadiliko ya hali
ya hewa na kutunza mazingira.
“Hatutajitenga katika dunia hii,
tutaendelea kujumuika katika kazi mbalimbali kama vile ulinzi wa amani,
kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhifadhi mazingira,’
alisema na kuongeza kuwa tumekuwa bandari ya amani kwa wakimbizi sio tu
kutoka Afrika bali duniani kote na tutaendelea kuwa hivyo,” Ameongeza
Prof. Kabudi.
Prof. kabudi pia amewataka
watumishi wa Wizara kusoma kitabu cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
alichowaandikia watumishi wa wizara hiyo mwaka 1969 cha Usipayuke toa
hoja ‘Don’t shout argue’ ili kutoa takwimu sahihi kwa wakati.
Amesema jukumu la kuieleza dunia
kuhusu takwimu za vitu mbalimbali ni la watumishi wa Mambo ya Nje na
hawana budi kuhakikisha wanaliekeleza hilo kwa ufasaha.
Mbali na kitabu hicho, Prof.
Kabudi amewakabidhi wakurugenzi wa Idara mbalimbali Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), hotuba za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati anafungu Bunge la 11 na hotuba
ya ufunguzi wa Bunge la 12 na kuwataka kusimamia na kutekeleza maagizo
yote yaliyopo kwenye hotuba hizo pamoja na maelekezo ya Ilani ya CCM.
Awali akimkaribisha Waziri
kuzungumza na watumishi, Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wibert Ibuge
aliwapongeza watumishi utendaji mzuri wa kazi na kuwataka kuendelea
kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
No comments :
Post a Comment