********************************
Na.Mwandishi Wetu -Arusha
Asasi kilele
inayojishughulisha na masuala ya maua,matunda,mboga mboga,Mimea
itokanayo na mizizi na Viungo (Horticulture),imedhamiria kuendelea
kukuza sekta hiyo kwa kufungua masoko ya kimataifa kwa wakulima hapa
nchini.
Akizungumza na vyombo
vya habari mkoani Arusha Mkurugenzi wa TAHA dkt.Jacquline
Mkindi,alisema kuwa taasisi hiyo imeandaa kongamano kubwa
litakalofanyika desemba 05 jijini dar es salaam katika hoteli ya Hyatt
Regency ijulikanayo Kama Kilimanjaro hoteli.
Dkt.Mkindi alisema
kuwa lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha fursa za uwekezaji wa masoko
katika mazao ya horticulture na majadiliano juu ya mazingira endelevu
ya kibiashara baina ya nchi zilizomo ukanda wa Afrika Mashariki na nchi
za ukanda wa kusini mwa Afrika(SADC).
Aidha alisema kuwa
washiriki watapata fursa ya kukutana na wadau wakubwa wa kilimo Cha
horticulture kwa nchi za Afrika Mashariki pamoja na SADC ili
kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya sekta hiyo na mawazo
ya kibiashara kati ya sekta binafsi na ya umma pamoja na wadau wengine
kwa lengo la kuvutia wawekezaji na pia kutengeneza ushirikiano linganifu
kati ya sekta ya horticulture Tanzania na zingine za kanda za
kibiashara za Afrika Mashariki na Kusini.
“Naikumbukwe kuwa
hivi karibuni wakati Raisi wetu Mhe.John Pombe Magufuli alitaja sekta ya
horticulture kuwa miongoni mwa sekta ndogo zinazokuwa kwa Kasi
nchini,ambapo alisema hivi Sasa nchi yetu inashika nafasi ya 20 kwa
kuzalisha kwa wingi mazao hayo duniani na mauzo yetu ya nje yameongezeka
kutoka Dola za marekani milioni 412 mwaka 2015,hadi kufikia Dola za
Marekani milioni 779 mwaka 2018/2019.”Alisema dkt.
Jacquline
Pia alisema kuwa
baadhi ya maeneo ambayo yatakayojadili ni pamoja na fursa za
uwekezaji,masoko,sekta ya usafirishaji,mfumo wa baridi na viwezeshi
vingine vinavyosaidia upatikanaji wa masoko kama sehemu kuendeleza na
kukuza kilimo na sekta hii baina ya nchi hizo.
“Naomba nitoe wito
kwa Watanzania ambao ni wazalishaji, wafanyabiashara,
wasafirishaji,wasindikaji,na wadau wakubwa wa horticulture kujisajili
kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo wa aina yake,kupitia tovuti ya www.taha.or.tz kujifunza
na kuchangamka fursa zilizopo ili kuboresha shughuli za tasnia hii ya
horticulture kisha kuendelea kuchangia ukuaji wa Uchumi nchini.”Alisema
Dkt.Jacquline
Mpaka sasa Jumla ya
nchi za Tanzania ,Malawi,Rwanda,Kenya,Sudani,DRC Congo na Comoro
zitashiriki kongamano hilo,huku jumla ya washiriki 400 watahudhuria
mkutano huo.
Mwisho.
No comments :
Post a Comment