WAKATI kukiwa na hofu
ya kuwepo kwa matumizi ya mbegu za mazao ambazo zinatokana na Mbegu
Zilizoongezewa Vinasaba (GMO) Serikali imesema bado haijaruhusu matumizi
ya mbegu hizo hapa nchini kwa ajili ya uzalishaji ila kwa sasa
kinachoendelea ni utafiti.
Hayo yamesemwa
na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Joseph
Sokoine wakati akifungua kongamano la wazi la kujadili usalama wa mbegu
lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Taasisi Mwamvuli ya Kilimo Hai
Tanzania (TOAM) na Shirika linalojishughulisha na Baionuwai nchini
(TABIO).
Katika kongamano hilo
ambalo lilishirikisha wadau zaidi ya 300 kutoka nchi tano za Afrika
Kusini, Bokinafaso, Ivory Cost, Tanzania na Uswisi Naibu Katibu Sokoine
amsema taarifa za kuwepo matumizi ya mbegu za GMO zinapaswa kupuuzwa
Kwani hazina ukweli ila utafiti unaendelea.
Amesema Serikali
haina sababu ya kuficha taarifa iwapo kuna mbegu zinazotokana na GMO
hivyo kuwaomba wadau kutoa taarifa iwapo wana ushahidi wa kuwepo mbegu
hizo.
“Utafiti mbegu hizi
za GMO unafanyika katika shamba letu la Makutopora Dodoma, hatuzalisha
ila zipo kwa ajili ya utafiti, Serikali lazima tujiridhidhe kabla ya
kuruhusu kutumika au kutotumika naomba mmpuze taarifa kuwa mbegu hizo
zinatumika,” amesema Sokoine.
Amesieitiza kuwa Tanzania kuna Sera ambayo inatambua teknolojia
ya inayoleta maendeleo kwenye kilimo lakini pia Sera inayotambua kilimo
endelevu hivyo ni jukumu la wadau kwenda pamoja kwa maslahi ya nchi na
wananchi.
Sokoine amesema uwepo wa mijadala kama hiyo juu ya usalama wa
mbegu itasaidia kwa kiasi kikubwa kuona njia sahihi ya kuifuata katika
utunzaji na uwendelezaji wa mbegu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi
kijacho.
Naibu Katibu Mkuu
huyo amesema Serikali inapenda kuona taasisi kama TOAM na TABIO kuleta
mijadala ambayo inagusa maisha ya Watanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa maendeleo ya mazao kutoka Wizara ya
Kilimo, Beatus Malema, amesema Serikali inaunga mkono kilimo endelevu
nchini (Kilimo hai) na kuwataka watu kuwekeza kwenye pembejeo ili
kuongeza tija ya uzalishaji.
Malema amesema kilimo hai kinatunza ardhi jambo ambalo
litapunguza kama sio kuondoa matumizi ya kemikali wakati wa msimu wa
kilimo ili kuongeza uzalishaji.
“Tunatambua mbegu za
asili ndio chanzo cha mbegu zote zikiwemo zinazobadilishwa vinasaba
hivyo kuna haja kubwa ya kuzitunza kwa ajili ya vizazi vijavyo lakini
pia zinachochea uzalishaji msingi,” amesema.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa TOAM, Dk. Mwatima Abdallah Juma
akizungumzia kongamano hilo amesema kuwa duniani kwa sasa kuna msukumo
mkubwa wa matumizi ya GMO hali inayohatarisha usalama wa mbegu za asili
hivyo ni jukumu la wadau wa kilimo hai kuungana na Serikali kupinga
mbegu hizo kwa kuwa sio salama kwa mlaji.
Dk.Juma amesema kongamano hilo litatoa nafasi kwa wakulima kuona umuhimu wa mbegu za asili na zinazoitwa za GMO.
“Sisi tunaamini mbegu
za asili ndio suluhisho la kuongeza uzalishaji zaidi kama watu
watafuata kanuni za kilimo bora na kilimo endelevu pamoja na kuwa kila
mkulima ana chaguo lake,” amesema Dk Juma.
Wakichangia katika
kongamano hilo lililofadhiliwa na Ubolozi wa Ufaransa na Uswisi baadhi
ya wadau wa kilimo waliweka wazi kuwa kilimo salama na endelevu ni
kutumia mbegu asili.
Wamesema dunia
inapaswa kuwa kauli moja katika suala la mbegu na kilimo kwani sekta
hiyo ni muhimu kwa maendeleo, kiuchumi, kisiasa na kijamii.
“Kukiwa hakuna
usalama wa mbegu ni wazi kuwa hata wa chakula hautakuwepo hivyo ni
jukumu la wadau wote kuwa pamoja katika kupigania mbegu asili,” amesema
mdau mmoja wa kilimo.
No comments :
Post a Comment