Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Philemon Sengati akifungua jana sherehe fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa Wakandarasi na Wakala wa barabara na Vijijini na Mijini (TARURA).
Mratibu wa Wakala wa barabara na Vijijini na Mijini (TARURA) Fibert Mpalasinge akitoa maelezo mafupi jana kabla ya kusaini mikataba ya matengenezo na ukarabati wa barabara mkoani Tabora na Wakandarasi 34 walioshinda zabuni.
……………………………………………
NA TIGANYA VINCENT
JUMLA ya shilingi bilinoni 5.4 zinatarajiwa kutumika katika ukarabati na kutengeneza
barabara za Mkoa wa Tabora ambazo ziko chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Philemon Sengati wakati wa sherehe fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa Wakandarasi na TARURA.
Alisema kiasi hicho ni awamu ya kwanza ya kiasi cha shilingi bilioni 7.1 iliyoidhinishiwa TARURA kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 kwa ajili ya matengenezo ya barabara.
Dkt. Sengati alisema kazi zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa kilimote 2.76 kwa kiwango cha lami , ujenzi wa makaravati zaidi ya mistari 59 na uchongaji wa barabara zaidi ya kilometa 541.
Aliwasihi Wakandarasi 34 walioshinda zabuni ya kutengeneza na kukarabati barabara hizo kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria , kanuni na miongozo , ubunifu na weledi ili Serikali iendelee kuwa na imani nao na kuwapa kazi zaidi.
“Wakandarasi waliomba kazi ni wengi lakini nyine 34 tu ndio mmefanikiwa kupata nafasi …kwa hiyo msituangashe …tangulize mbele uzalendo kwa maslahi mapana ya Mkoa wa Tabora na Taifa kwa ujumla” alisisitiza.
Aliwataka Wakandarasi walioshindika kazi hiyo kuhakikisha kazi inakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alimwagiza Mratibu wa TARURA na Wataalamu wake kuhakikisha wanasimamia kwa karibu miradi yote iliyopangwa ili ikamilike kwa viwango vilivypangwa.
Alisema Serikali inatoa fedha nyingi kwa miradi ya barabara , hivyo haitasita kumchukulia hatua Mtumishi ambaye atasababisha miradi kutekelezwa chini ya kiwango kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo.
Dkt. Sengati alisema ujenzi wa miundombinu hiyo na mingine itachochea maendeleo katika sekta za utalii, kilimo.mifugo, uvuvi , viwanda na biashara.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha kipato cha wakazi na Mkoa kwa ujumla na kufikia maono ya miaka mitano ijayo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi kwa wasatani wa asilimia 8 .
No comments :
Post a Comment