Katibu
Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
akielezea utekelezaji wa Afua mbalimbali za Kutokomeza Ukatili dhidi ya
Wanawake na Watoto nchini wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga
Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia
Ackson (kushoto) akiangalia muonekano wa GBV APP iliyotengenezwa kwa
ajili ya kupata taarifa za Ukatili wa Kijinsia wakati wa Uzinduzi wa
Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es
Salaam kulia mwenye koti ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia
Ackson akiwa katika picha ya pamoja pamoja na wanaharakati wa Mapambano
dhidi ya Ukatili wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi
ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam wa pili kushoto waliokaa ni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John
Jingu.
Baadhi
ya Wadau wakifuatilia masuala mbalimbali katika Uzinduzi wa Siku 16 za
kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
******************
NA EMMANUEL MBATILO
Serikali
inaendelea na mikakati ya kuhakikisha inapambana na Kutokomeza vitendo
vya Ukatili wa kijinsia kupitia mpango wa kamati ya kutokomeza ukatili
wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini ambao umelenga ifikapo 2022
Vitendo hivyo viwe vimepungua kwa asilimia 50.
Ameyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson wakati akizindua Kampeni ya Siku
16 za kupinga Ukatili wa kijinsia ikiongozwa na Kauli mbiu isemayo
"Tupinge vitendo vya Ukatili Mabadiliko yananza na mimi" uliofanyika
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumzia
utekekezaji wa Mipango mbalimbali ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John
Jingu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau katika
kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na Watoto
vinatokomezwa nchini.
No comments :
Post a Comment