
Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewaelekeza baadhi ya Wakazi wa eneo
la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya
tope linalofuka kutoka ardhini kuhama Mara moja ili kujikinga na maafa
wakati Serikali inaendelea kufanya utafiti wa kujua ukubwa wa eneo
lililoathirika.
Mapema leo RC Kunenge
akiongozana na wajumbe wa kamati ya usalama ya Mkoa wamefika Katika
eneo hilo na kushuhudia uwepo tope linalotoka ardhini na kupanda Katika
uso wa ardhi jambo lililosababisha baadhi ya nyumba kutitia, kupasuka
nyufa na mifugo kutitia jambo lililosababisha taharuki kwa wakazi wa
eneo hilo.
Kutokana na hali hiyo
RC Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuweka
alama za hatari Katika eneo hilo wakati Serikali chini ya taasisi ya
Geologia na utafiti wa Madini Tanzania ukiendelea kupia ukubwa wa eneo
lililoathirika.
Pamoja na hayo RC
Kunenge amesema Serikali inaangalia utaratibu wa kuwapatia wananchi wa
eneo hilo Viwanja vingine ili waweze kuendelea na maisha kama awali.
Kwa upande wake
Mtafiti kutoka taasisi ya Geologia na utafiti wa Madini Bwana Gabriel
Mbogoni amesema matokeo awali wamebaini chanzo Cha tope hilo ni
mgandamizo uliosababishwa na uwiano wa maji na chembechembe za udongo
kuharibika na kusababisha tope ambalo linasukumwa kutoka chini kwenda
kwenye uso wa ardhi.
Aidha Bwana Mbogoni amesisitiza kuwa tope hilo wamelipima na kukuta likiwa na joto la kawaida hivyo halina uhusiano wowote na ile volcano inayorusha majivu na Moto utokanao na miamba iliyoiva hivyo eneo hilo kwa Sasa ni tete na halifai kwa shughuli za Ujenzi Wala makazi.
No comments :
Post a Comment