‘Nilikuwa nafuatilia uchaguzi kupitia Television nikaona mama mmoja wa Ilemela ameshinda kwa kishindo, mara nikaona tena Hai nako CCM imeshinda, nikasema sasa kazi nzuri imefanywa na CCM” ,Amesema Museven
“Wengine wanafikiri ni jambo rahisi, lakini Afrika kufaulu lazima tukumbuke jambo la mwelekeo wa kisiasa, baada ya uhuru viongozi wetu waligawanyika, wengi wa Afrika walichukua mstari wa kuwa vibaraka wa nchi za nje wachache wakiongozwa na mwalimu Nyerere (Julius- Rais wa kwanza wa Tanzania) na wengine kama kina Mzee Kaunda na Seretse Khama walikataa.
"Kama tungefuata mstari ule mwingine wa vibaraka hawa viongozi hawangekuwa hapa, Kusini ya Afrika yote ilikuwa chini ya wakoloni kwa hiyo mnisamehe kuwa natazama TBC 1 kujua inakwendaje uchaguzi wa 2015 nilikuwa na hofu sana hii imekuwaje? Lakini baadaye nikaona alichaguliwa kwa kura nyingi sana.”
“Safari hii nikaona tena kule Hai nikasema heee Hai, hata Ilemela haya ndiyo majimbo ambayo walitangaza kwanza Newala huko nikasema aah basi, sasa mwisho naona nikiangalia umati wa watu hapa naona vijana wengi sana lakini vijana lazima mrithi msimamo wa wazalendo ambao walitangulia wakiongozwa na Mwalimu Nyerere.” - Amesema Museven
No comments :
Post a Comment