Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli amewaeleza
wananchi wa Tanzania kuwa uchaguzi mkuu umemalizika na jukumu lililopo
mbele ni kuwatumikia wananchi.
Rais
Magufuli amesema hayo leo Alhamisi tarehe 5 Novemba 2020 baada ya
kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma kuwa Rais wa
Taifa hilo, sherehe iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Pia,
Samia Suluhu Hassan, ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania ambao
kwa pamoja watawaongoza Watanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano
2020-2025.
Dk.
Magufuli ameapishwa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza
mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28
Oktoba 2020 kwa kupata kura milioni 12 kati ya milioni 15 zilizopigwa
sawa na asilimia 84.
Rais
Magufuli amewashukuru watu mbalimbali waliojitokeza kwenye sherehe
hizo, “nawashukuru sana na mimi kuwa Rais wa kwanza kuapishwa katika
hili Jiji la Dodoma.”
Huku
akishangiliwa, Rais Magufuli amesema “nawashukuru Watanzania wenzangu
kwa kuniamini na kunichagua ili niwaongoze kwa miaka mitano na kukipa
ushindi mkubwa chama changu cha mapinduzi na ushindi huu si wa wana CCM
pekee bali ni wa Watanzania wote”
Pia,
ameipongeza, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusimamia uchaguzi huu
pamoja na kuvishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kudumisha amani
kabla na baada ya uchaguzi.
Rais
Magufuli amesema, baadhi ya nchi, uchaguzi umekuwa chanzo cha mgogoro
na uhasama, “sisi Watanzania tumevuka salama na hii ni ishara kwamba
mwenyezi Mungu ametuvusha salama kama alivyotuvusha kwenye janga
corona.”
“Nawashukuru
viongozi wa mataifa mbalimbali waliokuja kuungana nasi, wapo marais,
mawaziri wakuu, mawaziri na mabalozi wote na wawakilishi wa taasisi za
mataifa kama EAC na SADC,” amesema Rais Magufuli.
Kiongozi
huyo amesema “uchaguzi sasa umekwisha, uchaguzi sasa umekwisha,
uchaguzi sasa umekwisha na jukumu kubwa na muhimu lililopo mbele ni
kulijenga na kuleta maendeleo taifa letu na niwahakikishe Watanzania,
kiapo nilichoapa na makamu wangu (Samia Suluhu Hassan), tutakienzi.”
Rais
Magufuli amesema, katika uongozi wa miaka mitano, watasimamia kumaliza
miradi waliyoianzisha, kusimamia rasilimali mbalimbali za taifa,
kushughulikia tatizo la ajira hususan vijana na kero zinazowakabili
wananchi na kuzidisha mapambano ya rushwa na ufisadi.
No comments :
Post a Comment