Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mtumishi wa Idara ya Chumba
cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Madaraka
Joseph (32) na Mmiliki wa Zahanati ya Suka ( Suka Wazazi Dispensary) ,
Dk. Suka Charles kwa tuhuma ya wizi wa vifaa tiba zikiwemo mashine za
kuangalia wagonjwa zenye thamani ya shilingi milioni 26 katika hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari leo,Jumamosi Novemba 7,2020, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema wizi huo
umetokea Oktoba 13,2020 majira ya saa 10 jioni katika hospitali ya Rufaa
ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda
Magiligimba amesema Oktoba 13,2020 kulitokea wizi wa mashine mbili za
kuangalia wagonjwa katika chumba cha upasuaji aina ya EDAN 1M8 na DATA
SCOP 1 zenye thamani ya shilingi milioni 26 mali ya Hospitali ya Rufaa
ya mkoa wa Shinyanga.
“Kufuatia
tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga likaanza uchunguzi wake
mara moja na kubaini kuwa mtuhumiwa Madaraka Joseph, Muuguzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na mkazi wa Mageuzi Mjini
Shinyanga ambaye ni Mtumishi wa Idara ya Chumba cha Upasuaji ndiye
aliyeziiba mashine hizo na kwenda Kuuza kwa Dk. Suka Charles ambaye ni
Mmiliki wa Suka Dispensary iliyopo wilayani Kahama ambaye ni mkazi wa
Buzuka Mjini Shinyanga na makazi mengine wilayani Kahama”,ameeleza Kamanda Magiligimba.
“Muuguzi
huyo wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Madaraka Joseph aliuza
mashine hizo kwa Suka Charles kwa makubaliano ya Shilingi Milioni 4
ambapo alishatanguliziwa shilingi milioni 2”,amesema Kamanda Magiligimba.
Kamanda
huyo wa polisi amesema baadae Suka Charles alikamatwa na upekuzi
ulifanyika nyumbani kwake maeneo ya Mhongolo wilayani Kahama na
kufanikiwa kupata mashine hizo (EDAN 1M8 na DATA SCOP 1) zikiwa na vifaa
vyake.
Amevitaja
vifaa hivyo kuwa ni Patient Monitor mbili, BP mashine accessories
5,cable wires accessories 7,medical molecular sieve,Oxygen Concentrator
na Oxygen Concentrator Intesty.
Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Ametoa
wito kwa watumishi kuacha tabia ya wizi wa mali za umma zinazotokana na
tama ya mafanikio ya muda mfupi ambapo hupelekea wananchi kukosa huduma
hivyo kuibebesha lawama serikali.
Hata
hivyo amesema Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga litaendelea kuchukua
hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote au watumishi wa serikali
watakaobanika kufanya uhalifu wa aina yoyote ile.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari leo Jumamosi Novemba 7,2020 kuhusu wizi wa vifaa tiba
uliotokea Oktoba 13,2020 majira ya saa 10 jioni katika hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa tiba
mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika
Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya
vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa
katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Muonekano
wa sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni
26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment