Mkurugenzi wa Rasilimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi
Mary Mwangisa, akitoa maelekezo wa baadhi ya watalaam watakaoshiriki
katika elimu ya mafunzo na matunzo ya miondombinu ya umwagiliaji kwa
wakulima.
Mkurugenzi msaidizi wa idara ya mafunzo na matunzo kutoka Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni akifafanua jambo wakati wa kikao na
wataalam,cha maandalizi ya utoaji elimu kwa wakulima kuhusiana na
utunzaji wa miundominu ya Umwagiliaji.kulia, ni Bw.Reginald Diamett
Meneja Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji.
**************************************
Na MwandishiWetu Dodoma
Mkurugenzi Rasimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Mary Mwangisa, amewapa maekelezo baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo watakaoshiriki katika zoezi la utoaji elimu na mafunzo ya utunzaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliji katika baadhi ya skimu za kilimo hicho
nchini.Akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Bi Mwangisa amesema kuwa watumishi hao wanapaswa kuzingatia mwongozo wa namna ya kutoa mafunzo ya vyama vya umwagiliaji wa namna ya kukusanya mapato kwa ajili ya uchangiaji wa mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji, matumizi sahihi ya kalenda za kilimo na utunzaji wa miundombinu ya umwagiaji.
“Serikali imewekeza pesa nyingi katika miundombinu ya umwagiliaji kwa hiyo isipotunzwa serikali itapata hasara, na wakulima wataathirika, vyama vya umwagiliaji vitakufa na miundombinu hiyo itakufa.” Alisisitiza.
Aliendelea kusema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni moja kati ya mategemeo ya kuongeza uzalishajiwa mazao ya chakula na biashara na uhakika wa usalama wa chakula nchini.
Maelekezo hayo kwa watumishi yametolewa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkakati wa tume ya taifa ya umwagiliajiwa kutoa elimu kwa vyama vya umwagiliaji nchini.
No comments :
Post a Comment