Mkaguzi wa Michezo ya
Kubahatisha Kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Joram
Mtafya (kushoto) akichagua kuponi wakati wa bahati nasibu ya mawakala wa
konyagi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,(Kulia) ni
Meneja Usimamizi wa kanda za Mauzo wa TDL, Mwesige Mchuruza.
Baadhi ya pikipiki za usambazaji ambazo mawakala wamejishindia.
Meneja wa kiwanda cha
Konyagi, Aranyaeli Ayo (kulia) akikata utepe kuzindua mchezo wa bahati
ya mawakala wa kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam ambapo
wawakala 4 wamejishindia pikipiki za matairi 3,kushoto kwake ni Meneja
Usimamizi wa kanda za Mauzo wa TDL, Mwesige Mchuruza.
……………………………………………………………………….
Mawakala wanne wa kampuni ya Tanzania
Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu
cha Konyagi na jamii zake, wanaofanyia biashara zao katika mikoa
mbalimbali nchini, wamejishindia pikipiki zenye magurudumu matatu za
usambazaji kila mmoja baada ya kuibuka washindi katika kampeni ya mauzo
ya miezi 3 ambayo ilikuwa inaendeshwa na kampuni kuanzia mwezi Julai
mpaka Septemba mwaka huu.
Bahati nasibu ya kuwapata washindi ilifanyika
katika kiwanda cha Konyagi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki chini
ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha na kuhudhuriwa
na na maofisa mbalimbali kutoka kampuni hiyo.
Akiongea wakati wa bahati nasibu hiyo,Meneja
Usimamizi wa kanda za Mauzo wa TDL,Mwesige Mchuruza ,alisema kuwa
kampeni hiyo iliyolenga kuwawezesha mawakala wa kampuni wanaouza
kinywaji cha Konyagi imefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu na mawakala
64 walifikia vigezo vya kuingia katika shindano ambapo miongoni mwao
wanne wameshinda kupitia bahati nasibu na wamefanikiwa kujishindia
pikipiki za kubeba mizigo.
Aliwataja mawakala walioibuka na ushindi kuwa ni
Victoria Simba Ufoo (kanda ya kusini), Nkamba Zephania Masaladi- (Kanda
ya Kaskazini Magharibi), Yatenga Company- (Nyanda za Kusini) na Agness
Method Mtenga- (Kaskazini Mashariki).” Ni faraja yetu kubwa tukiona
huduma za bidhaa zetu zikiboreshwa kila mara na kuwafanya wasambazaji
wetu wawe na motisha ya kuendelea kufanya kazi na sisi tunawashukuru
wote walioshiriki,” alisema Mchuruza.
Aliongeza kuwa kampeni hii ni mwendelezo wa
kampeni za kampuni kupitia mpango wa kuwaendeleza wafanyabiashara
wanaosambaza bidhaa zake, mbali na kuwapatia zawadi vifaa vya
kuwarahisishia usambaza pia imekuwa na utaratibu wa kuwapatia mafunzo
mbalimbali kwa ajili ya kukuza biashara zao.
No comments :
Post a Comment