Wednesday, November 25, 2020

MAKABIDHIANO YA OFISI WIZARA FEDHA NA MIPANGO YAFANYIKA ZANZIBAR

Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na
Mipango Khamis Mussa Omar akitoa hotuba ya makaribisho katika Mkutano
maalum wa Makabidhiano ya Ofisi na Kumuaga Waziri wa Fedha na Mipango
Mstaafu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa hafla iliofanyika katika ukumbi
wa Wizara hiyo Vuga Jijini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia
Abdiwawa (kulia) wakiweka  saini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha
na Mipango Jamal Kassim Ali katika Mkutano maalum wa Makabidhiano ya
Ofisi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga Jijini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia
Abdiwawa (kulia)akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na
Mipango Jamal Kassim Ali Nyaraka mbalimbali katika Mkutano maalum wa
Makabidhiano ya Ofisi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga
Jijini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Mstaafu Balozi Mohamed Ramia
Abdiwawa akitoa hotuba baada ya kumkabidhi  Waziri wa Nch,i Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali Nyaraka mbalimbali  katika hafla  maalum ya Makabidhiano ya ofisi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Vuga Jijini Zanzibar.

 Na Takdri Ali, Zanzibar

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Raisi Fedha na Mipango  Jamal Kassim Ali
amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo kutumia elimu walizonazo kwa
kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika Ofisi hiyo na Taifa kwa
ujumla.

Amesema Wizara hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya Wananchi hivyo ni vyema
Wataalamu wa fani mbalimbali waliomo kuwa Wazalendo na kuhakikisha
wanafikia malengo ya Serikali ya awamu ya nane ya kufikia uchumi wa
Bluu.

Waziri Jamal ameyasema hayo huko Ofisini kwake Vuga wakati wa
makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohammed
Ramia Abdiwawa aliyemaliza muda wake.

Amesema Timu ya uongozi aliokabidhiwa ni nzuri kwani inawataalamu
wengi na wa fani mbalimbali na kuahidi kuendeleza mwendo wa kasi
katika kuleta maendeleo.

Aidha amepongeza Waziri huyo mstaafu kutokana na kazi na jitihada
kubwa alizozichukuwa katika Uongozi wake na kuacha msingi mkubwa kwa
faida ya Wizara na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri Mstaafu wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi
Mohamed Ramia amesema maendeleo yaliyopatikana yametokana na
Ushirikiano wa Wafanyakazi wa Wizara hiyo hivyo ni muhimu kutoa
ushirikiano na Waziri mpya ili kuweza kuyaendeleza na kufanya kazi kwa
ufanisi.

Aidha amewakumbusha Wafanyakazi hao kufanya kazi kwa Uzalendo na
kutosahau kuwa wanatakiwa kuwa waaminifu na kuzingatia uwajibikaji
wa kazi zao.

Nao Wafanyakazi wa Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
wamemshukuru Waziri aliyemaliza muda wake kwa ushirikiano aliowapa na
kuahidi kushirikiana na Waziri mpya kwa maslahi mapana ya wananchi wa
Zanzibar.

 

No comments :

Post a Comment