Wednesday, November 25, 2020

BAADHI YA MAKAMPUNI YA SIMU YAANZA KUSAIDIA JAMII

Meneja mauzo wa Itel kanda ya kaskazini Maiga Pamba, akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na mkakati wao wa kurudisha fadhila kwa jamii ambayo ndio wateja wakubwa wa simu hizo, leo jijini Arusha.

Meneja Masoko wa Simu za mkononi za itel , Elfas Leiya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kusaidia jamii kupitia biashara hiyo ambayo sehemu ya faida itakayopatikana kwa kila simu itaelekezwa katika kundi husika, leo Jijini Arusha.


Na Woinde Shizza, Michuzi TV Arusha

BAADHI ya Makampuni ya Simu za mkononi nchini kupitia bidhaa zao mpya,
yameanza kuwa na mwamko wa kuisaidia jamii kwa kutoa msaada wa faida
kidogo inayopatikana na kuipeleka kwenye makundi yenye uhitaji ili
kusaidia jamii hiyo kupunguza umaskini nchini.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha na meneja Masoko wa Simu za mkononi
za itel , Elfas Leiya ,wakati wa hafla fupi ya kutambulisha sokoni Simu
Mpya aina ya itel S16 ,ambapo Kampuni hiyo imeamua kutoa sh. 1000 kwa
kila Simu ya aina hiyo itakaponunuliwa.

"Tupo hapa Arusha kutambulisha Simu Mpya aina ya itel S16 ambapo
katika Simu hii tutatoa sh, 1000 kwa kila Simu itakayouzwa ili
kuchangia makundi yasiyojiweza." amesema.

Leiya aliongeza kuwa Kampuni nyingi za Simu hapa nchini zimekuwa
zikivuna faida kubwa bila kujali jamii ambayo ndio wanunuzi wakubwa wa
bidhaa zao kwa kurudisha walau faida kidogo kwa Jamii.

Aidha amesema katika kipindi hiki cha mwezi wa kumi na moja
wanatarajia kuuza Simu za aina hiyo zipatazo 15,000 ambapo sehemu ya
mauzo hayo yatapelekwa kwenye vituo Vya watoto yatima kama mchango wao kwa Jamii hiyo .

Akiongelea sifa ya simu hiyo mpya aina ya Itel S16, meneja mauzo wa
kanda ya kaskazini Maiga Pamba amesema, wameamua kuitambukisha sokoni
simu hiyo mpya kutokana na uimara wake hasa  kukaa na chaji kwa muda
 wa wiki moja bila kuchajiwa unaotokana na uwezo mkubwa wa betri
yenye ukubwa wa  Megawatt 4000.

Pia amesema Simu hiyo imekuja kwenye ushindani wa soko la simu nchini
kwa lengo la kumsaidia Mwananchi mwenye  changamoto ya kuchaji ili
aweze kuwa na uhakika wa kuitumia muda wote .

 

No comments :

Post a Comment