Friday, November 20, 2020

GGML, NEEC WAANZISHA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA 500 GEITA

Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Richard Jordinson (kushoto)akitoa hotuba kwenye mafunzo hayo ya wafanyabiashara mkoani Geita. Kulia ni Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Joseph Mangilima akitafsiri hotuba hiyo kwa washiriki.
Katibu Mtendaji wa Barazala Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo (hawapo pichani)

Na Mwandishi wetu
Katika jitihada za kuwapatia maarifa na ujuzi wajasiriamalimkoani Geita juu ya mchakato wa manunuzi yanayofanywa na Kampuni ya Geita GoldMining Limited (GGML), kampuni hiyo imefadhili mafunzo maalum yanayoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Mafunzo hayo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwana GGML na NEEC Julai 20, mwaka huu kuhusu namna bora ya kuwasaidia wajasiriamalimkoani Geita ili wapate fursa bora ya kufanya biashara na taasisi mbalimbali nchiniikiwemo GGML.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa kituo cha uwekezaji mjini Geita, Mkurugenzi Mtendaji waGGML, Richard Jordinson alisema kampuni hiyo inalenga kuboresha ushiriki wa wafanyabiashara mkoani humo katika zabuni mbalimbali zinazotangazwa na kampuni hiyo.

Alisemamalengo hayo ni kuwajengea uwezo ili wafahamu vigezo muhimu na kutimiza matakwaya kisheria kusambaza bidhaa na huduma mbalimbali kwenye sekta ya uchimbaji madinisanjari na sekta zingine.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo ni uthibitisho tosha kuwa kampuni ya GGML inakusudia kuchochea maendeleo endelevu kwa jamii inayozungukamgodi.

“Tumeendelea kuthibitisha haya kwa vitendo kwa kushirikianana Serikali kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, miundombinu yabarabara pamoja na shughuli mbalimbali za kuwawezesha wananchi kiuchumi maeneo yanayozungukamgodi,” alisema Jordinson.

Alisema mpango huo unaotumia bajeti ya shilingibilioni 1.3 za Kitanzania, unawalenga wajasiriamali 500 wanaoishi mkoani Geita wakiwemovijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

“Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka2017, GGML kupitia fedha za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii imeshirikiana vyemana halmashauri mkoani Geita kutekeleza miradi ya maendeleo kwa jamii yenye thamaniya jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 30 mkoani Geita,” alisema Jordinson.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza laTaifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa aliipongeza GGML kwa mpangohuo ambao unaendana na mpango wa kuendeleza biashara mkoani humo.

“Mpango huu utawajengea uwezo na kujiamini wajasiriamalina kushindana vyema na wafanyabiashara wengine nchini ili baadaye waweze kuboreshamapato na maisha yao,” alisema Beng’i Issa.

 

No comments :

Post a Comment