Na John Walter-Manyara
Rais Dr. John Pombe Magufuli leo Novemba 12,2020 akihutubia
wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 Jijini Dodoma, amesema katika kipindi
cha miaka mitano katika usafiri wa anga, kutajengwa kiwanja Kikubwa
kipya cha Msalato, kufanya upanuzi na ukarabati wa Viwanja kumi na moja
(11) vikiwemo vya Kigoma, Shinyanga,Sumbawanga, Tabora, Mtwara, Songea.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa kutajengwa viwanja vya kutua na
kuruka ndege kwa kiwango cha lami kwenye Viwanja vya Iringa, Lake
Manyara, Tanga, Musoma, Lindi, Kilwa Masoko, Njombe,Singida,Simiyu na
kadhalika.
Mbali na hayo, Rais Dr. John Pombe Magufuli amesema atanunua Ndege mpya tano, moja ikiwa ni ya mizigo.
Mbali na hayo, Rais Dr. John Pombe Magufuli amesema atanunua Ndege mpya tano, moja ikiwa ni ya mizigo.
Aidha Dr. Magufuli amesema kuwa Mwaka huu wametunga sheria mpya
ya kusimamia na kuendeleza uvuvi wa bahari kuu ambapo wamepanga kununua
meli nane za uvuvi kwa kushirikiana na shirika la IFAD, meli hizo nane,
Nne zitakuwa upande wa Zanzibar na Nne zitakuwa upande wa Tanzania Bara
ambazo meli hizo zitashiriki katika uvuvi wa bahari kuu huku
wakikusudia kujenga bandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira elfu 30.
Katika Dr. Magufuli amesema ili kuvutia Uwekezaji, kwenye Sekta
ya viwanda wataendelea kuboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji
ikiwemo kuangalia masuala ya kodi na kuondoa vikwazo na urasimu ambapo
kumekuwepo na Urasimu mwingi na kusumbuliwa kwa wawekezaji kwa
kuzungushwa hali inayowafanya wakate tamaa.
Amesema anataka mwekezaji mwenye fedha akija apate kibali ndani
ya muda wa siku kumi na nne (14), na kwa sababu hiyo ameamua suala la
uwekezaji ikiwa ni pamoja na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)
kulihamishia kutoka ofisi ya waziri mkuu kwenda ofisi ya Rais ili
wanaokwamisha akapambane nao yeye mwenyewe.
Rais John Pombe Magufuli anaendelea kuongoza nchi ya Tanzania
katika awamu ya pili na ya mwisho ambapo awali aliingia madarakani
mwaka 2015 akiwa na kaumbi mbiu “HAPA KAZI TU” na sasa mwaka 2020-2025
akiongozwa na Kauli mbiu ya “ACHA KAZI IENDELEE
No comments :
Post a Comment