Na John Walter-Manyara
Kufuatia agizo la Rais Dkt.John Magufuli kwa Shirika la Umeme
Tanzania kuwaunganishia wananchi 4,000 Umeme katika mkoa wa Manyara,
Bodi ya Wakurugenzi TANESCO ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Alexander
Kyaruzi imefika mkoani hapo kufuatilia utekelezaji wa gizo hilo.
Agosti 25,2020 Rais Dr.John Pombe Magufuli akiwa katika kampeni
mjini Babati alitoa siku 30 kwa Tanesco mkoa wa Manyara kuhakikisha
wananchi 4,000 ambao tayari wamtimiza vigezo vya kupatiwa huduma ya
umeme wanapatiwa huduma hiyo.
Dkt. Kyaruzi amesema Kazi hiyo itafanyika usiku na mchana ili
ndani ya siku 30 watu 4,000 na ikiwezekana zaidi wawe wameunganishiwa
Umeme katika nyumba zao.
Amesema Tanesco Mkoa, Kanda na Makao Makuu wameweka nguvu kubwa
ili kuhakikisha agizo la Rais linatekelezwa kwa muda na ikiwezekana
wamalize kabla na kuongeza wateja zaidi ya hao wanaotakiwa kupatiwa
Umeme.
Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi TANESCO ilitembelea maeneo
mbalimbali ya wilaya ya Babati ambapo imeshuhudia shughuli za kuweka
nguzo ikiendelea.
Meneja wa Tanesco mkoa wa Manyara Mhandisi Rehema Mashinji
amesema uongozi wa shirika umetoa msaada mkubwa katika kuhakikisha
wananchi wanapata huduma ya Umeme ambapo mpaka sasa wameshapokea vifaa
mbalimbali huku nguzo zikisambazwa kwa nusu ya wateja 4000 wnaopaswa
kupata Umeme kwa awamu hii.
Amewataka Wananchi wawe wavulivu wakati huu wakiendelea kusambaza miundombinu ya Umeme katika maeneo yao ili huduma iwafikie.
Ameeleza kuwa Umeme huo unaousambazwa kwa sasa katika maeneo yao unagharamiwa na Tanesco na sio REA.
Kwa Mujibu wa Meneja wa Tanesco mkoa wa Manyara Mhandisi Rehema Mashinji Shirika katika mkoa huo linawahudumia wateja 41,500.
Mzee Emmanueli Kasmiri ameipongeza bodi ya wakurugenzi wa
Tanesco kufika mkoani Manyara na kukagua miundombinu ya Umeme kwa kuwa
itaongeza kasi kwa watendaji wa shirika hilo katika kuwapatia Umeme kwa
kuwa ni muda mrefu walikuwa gizani.
No comments :
Post a Comment