Monday, October 5, 2020

Wizara ya Fedha Kuimarika Kielektroniki

********************************************

Na.Epifania Gustafu-MAELEZO

Serikali imewaagiza maafisa masuhuli wote wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuhakikisha kuwa mpango wa bajeti kwa mwaka 2021/2022 unaandaliwa kwa mfumo mpya wa

uandaji wa bajeti,( PlanRep).

Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa uandaaji wa bajeti jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mary Maganga, alimemtaka Msajili wa Hazina Athumani Mbutuka kutochambua bajeti yoyote itakayowasilishwa nje ya mfumo huu.

Pia amempongeza Msajili huyo kwa utekelezaji wa mfumo huo ambao ni matokeo ya juhudi zilizofanywa na ofisi yake katika kuimarisha usimamizi wa fedha za umma katika Wakala za Serikali.

Aidha amewashukuru wadau wa maendeleo wanaofadhili Mradi wa Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) kwa kuwezesha kifedha ujengaji wa mfumo huo na kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali katika kuimarisha nchi.

“Nawapongeza kwa dhati vijana wetu, Watanzania wenzetu, ndani ya Serikali kwa weledi wao na jitihada zao zilizosababisha kufanikisha kujenga customization ya mfumo huu, hongereni sana hatuna budi kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano , kwani mafanikio yote haya yamewezekana chini ya uongozi wake thabiti na imara”, Amesema Maganga.

Ameongeza kuwa uwepo wa mfumo huo utapunguza upotevu wa mapato, kuimarisha na kuchochea uwajibikaji, kuimarisha uchambuzi wa bajeti na ufuatiliaji na hatimaye kuongeza mapato katika mfuko Mkuu wa Serikali.

“Nafahamu ofisi yako haikuwa na mfumo ambao ungeiwezesha kufualitia utekelezaji wa bajeti za Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Hivyo basi, mfumo huu utakuwa kitendea kazi muhimu cha ofisi yako na naamini hata Wizara na Taasisi nyingne za Serikali kuu zitaweza kutumia mfumo na kuweza kuokoa gharama ambazo zinalipwa kwa ajili ya mfumo wa kibajeti” .Amesema Maganga.

Amebainisha kuwa mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa ulipaji Serikalini (MUSE) na kuwezesha kudhibiti matumizi ya fedha za umma nje ya mipango na bajeti iliyoidhinishwa.

Kwa upande wa Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka amesema Ofisi hiyo ikishirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Fedha na Mipango katika mwaka wa Fedha 20219/20 ilianzisha mradi wa kusimika Mfumo wa uandaaji na uwasilishaji wa bajeti Kielectronik (PlanRep) utakaotumika katika Wakala za Serikali,Taasisi na Mashirika ya Umma.
Mwisho.

 

No comments :

Post a Comment