Monday, October 5, 2020

WIKI YA WAWEKEZAJI DUNIANI YAANZA RASMI LEO, MAMLAKA KUWAJENGEA UWEZO WATANZANIA KUFAHAMU UMUHIMU WA FURSA ZILIZOPO


Afisa
Mtendaji Mkuu Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
CPA,Nicodemus akizungumza na kuzindua wiki ya kimataifa ya Uwekezaji
Duniani mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar,ambapo CMSA itatumia maadhimisho hayo kuendelea kuelimisha Umma wa
Watanzania kuhusu kutambua fursa zilizopo na jitihada zinazoendelea za
masoko ya mitaji na kuweka mazingira bora, shirikishi na endelevu ya
kisera, sheria na utendaji. 
Baadhi
ya Wageni waaliakwa mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi
wa Wiki ya kimataifa ya Uwekezaji Duniani inayoratibiwa na MAMLAKA ya
Masoko ya Uwekezaji wa Mitaji ya Masoko na Dhamana (CMSA) hapa nchini. 
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja (UTT-AMIS,Simon
Migangala akieleza mbele ya Wanahabari leo jijini Dar, namna
watakavyoshiriki kutoa elimu kuhusu Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa
Wadau mbalimbali katika Wiki ya kimataifa ya Uwekezaji Duniani
inayoratibiwa na MAMLAKA ya Masoko ya Uwekezaji wa Mitaji ya Masoko na
Dhamana (CMSA) hapa nchini. 
Mwakilishi
wa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam,Brighton Kinemo
akieleza mbele ya Waahabari leo jijini Dar, namna watakavyoshiriki 
kutoa elimu kuhusu soko la hisa kwa Wadau mbalimbali katika Wiki ya
Kimataifa ya Uwekezaji Duniani inayoratibiwa na MAMLAKA ya Masoko ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Masoko na Dhamana (CMSA) hapa nchini.
Mwenyekiti
wa chama cha Watendaji wa Soko la Hisa la Dar es Salaam
(TSEBA),Bwa,Gerase Kamugisha akizungumza mbele ya Waandishi wa habari
(hawapo pichani),leo jijini Dar namna watakavyoshiriki wiki ya Kimataifa
ya Uwekezaji Duniani inayoratibiwa na MAMLAKA ya Masoko ya Uwekezaji wa
Mitaji ya Masoko na Dhamana (CMSA) hapa nchini.

 Na Mwandishi Wetu ,Michuzi TV
 
MAMLAKA
ya Masoko ya Uwekezaji wa Mitaji ya Masoko na Dhamana imeanza wiki ya
kimataifa ya Uwekezaji Duniani ambapo itatumia maadhimisho hayo
kuendelea kuelimisha Umma wa Watanzania kuhusu kutambua fursa zilizopo
na jitihada zinazoendelea za masoko ya mitaji na kuweka mazingira bora,
shirikishi na endelevu ya kisera, sheria na utendaji.
 
Juhudi
hizo zinalenga kukuza Uwekezaji kupitia masoko ya mitaji, hivyo
kuchochea kwa uchumi nchini Tanzania huku ikielezwa kwamba mpaka sasa
Uwekezaji katika masoko ya mitaji ni Sh.trilioni 27 ambapo uwekezaji
katika hisa ni Sh.trilioni 15 ,hati fungani ni Sh.trilioni 11.5 na
mifuko ya Uwekezaji wa pamoja ni Sh.Bilioni 500.
 
Hayo
yamesemwa leo Oktoba 5,2020 jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu
Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) CPA,Nicodemus Mkama
wakati akizungumzia Wiki ya Kimataifa ya Maadhimisho ya Wawekezaji
Duniani kwa mwaka 2020 yenye kauli mbiu inayosema ambapo kauli mbiu
inasema kuongeza uelewa na kulinda maslahi ya wawekezaji katika masoko
ya mitaji.
 
Amefafanua
kuwa Wiki ya Wawekezaji Duniani inaadhimishwa Kimataifa kwa kuratibiwa
na Taasisi ya ushirikiano wa mamlaka za Usimamizi wa Masoko na Mitaji
Duniani ambayo kwa kifupi inajulikana kwa IOSC na kwamba pamoja na
majukumu mengine IOSC imeweka kanuni zenye vigezo vya kimataifa vya
Usimamizi wa masoko na mitaji Duniani ili kuwezesha nchi mbalimbali
kusimamia na kuratibu sekta ya masoko na mitaji kwa lengo la kuepusha
athari za utandawazi kea kuzingatia vigezo vya Kimataifa na ushirikiano
kati ya nchi wanachama.
 
“Kwa
mantiki hiyo IOSC inaratibu shughuli za wiki ya maadhimisho hayo
Duniani kwa lengo la kuongeza uelewa umuhimu wa elimu ya wawekezaji kwa
umma na kulinda maslahi ya wawekezaji kwa kutumia njia na mbinu
mbalimbali. Aidha kushiriki katika shughuli hiyo kunawezesha wadau
mbalimbali katika sekta ya masoko ya mitaji kufanya kazi kwa pamoja
katika nchi zao na Kimataifa.
 
“Katika
kutekeleza azma hiyo CMSA inaadhimisha wiki hii kwa kushirikiana na na
wadau mbalimbali katika masoko ya mitaji na ndio maana wanawaona Mfuko
wa Uwekezaji wa pamoja wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu ,pia wapo Soko
la hisa pamoja na watendaji katika masoko ya mitaji na kampuni ambazo
zimepewa leseni kutoka Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana.
 
“Kwa
hiyo tunaanza rasmi leo kuadhimisha wiki hii hadi Ijumaa kwa lengo kuu
moja kuwa na programu ambazo zitaongeza uelewa kwa wananchi kuhusu
masoko ya mitaji ili kuwezesha kuongeza Uwekezaji na kulinda maslahi ya
wawekezaji, hivyo kuongeza mchango wa sekta ya masoko ya mitaji katika
kukuza uchumi nchini,”amesema.
 
Ameongeza
kuwa shughuli ambazo zitafanyika katika wiki ya maadhimisho hayo
zitajumuisha kutoa elimu kwa wawekezaji na wananchi kwa ujumla kuhusu
umuhimu wa masoko ya mitaji katika uchumi, bidhaa mbalimbali
zinazotolewa katika masoko ya mitaji, namna ya kupata mitaji kupitia
masoko hayo,jinsi ya kushiriki kuwekeza katika masoko ya mitaji.
 
“Programu
hiyo inalenga kuongeza bidhaa za kuwekeza na kuongeza matumizi ya
masoko katika upatikanaji wa mitaji katika shughuli za uchumi na kupanua
wigo wa Uwekezaji.Tukio hili ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati
wa mamlaka wa miaka mitano ambao pamoja na mambo mengine tunapanga
kuendeleza masoko ya mitaji Tanzania ikiwa pamoja na kutoa elimu ya
masoko ya mitaji na dhamana kwa makundi mbalimbali,”amesema. 
 
Pia
mkakati huo unalenga kujenga uwezo watendaji lakini na kuongeza uelewa
wa umma kuhusu fursa na manufaa yanayopatikana kwa kuwekeza katika
masoko ya mitaji huku akifafanua wawekezaji na washiriki katika masoko
ya mitaji wanahitaji kupata uelewa wa kutosha kuhusu masoko ya mitaji na
namna ya kushiriki katika hatua muhimu ya kuwawezesha kulinda maslahi
yao na kufanya uwekezaji endelevu na hilo ni jukumu mojawapo la mamlaka
hiyo kuhakikisha wanatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria.
 
“Tukizingatia
kwa sasa hivi Tanzania inatekeleza sera ya uchumi wa viwanda ,mahitaji
ya mitaji kwa shughuli za uchumi yanaongezeka , kwa hiyo ni dhahiri
kujenga uwezo na ushirikiano wa pamoja kama wadau wakuu katika sekta ya
masoko ya mitaji kuwezesha wahitaji wa mitaji kupata fedha hizo katika
sekta hiyo kuongeza wigo wa kuwekeza Umma wa Watanzania.
 
“Ikumbukwe
masoko ya mitaji yanatumika kukuza uchumi wa nchi kwa kuwezesha
shughuli za uchumi kukua, kampuni kupata mitaji na kuongeza nafasi za
ajira, kuongezeka kwa kodi stahiki za Serikali na kuwezesha Serikali
kuboresha huduma za jamii na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kwa
jamii nzima kwa ujumla,”amesema.
 
Hata
hivyo amesema mpaka sasa uwekezaji katika masoko ya mitaji ni trilioni
27 ambapo uwekezaji katika hisa ni trilioni 15 ,hati fungani ni trilioni
11.5 na mifuko ya Uwekezaji wa pamoja ni Bilioni 500.”Kwa hiyo mnaweza
kuona kwa kiasi gani sekta hii ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa
uchumi hapa nchini.
 
“Elimu
ya uwekezaji na uelewa wa masoko ya mitaji kunawezesha wananchi kwa
ujumla kuepuka kushiriki katika fursa za uwekezaji ambazo sio halali na
wenye udanganyifu kwani siku za karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa kwa
umma kutapeliwa na kushiriki kwenye danganyifu ,hivyo kwa kutumia
maadhimisho hayo tutaendelea kutoa elimu Umma kuhusu sekta hii na
umuhimu wa ushiriki wao.”

No comments :

Post a Comment