Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kulia
anayeandika) akikagua moja ya kazi inayofanywa na mkandarasi kampuni ya
Musons Engeneers Ltd inayotekeleza mradi wa maji mjini Chato. Mhandisi
Kemikimba akikagua kazi zilizofanyika katika mradi amewataka wakandarasi
kufanya kazi kwa saa 24 ili wananchi na taasisi za umma ikiwemo shule
na hospitali zipate maji ya kutosha kwa shughuli mbalimbali za maendeleo
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kulia)
akiangalia mtambo wa kusukuma maji katika chanzo cha maji cha Rubambagwe
ambacho kimefanyiwa maboresho ili kuimarisha huduma ya maji kwa
wananchi wa Chato.
Mhandisi
Jackson Kyelekule kutoka kampuni ya Musons Engeneers Ltd akionyesha
hatua zilizofanyika katika ujeni wa tanki la kuhifadhi maji, ujenzi huo
unaendelea na utakamilika mwezi Novemba hivyo kuimarisha hali ya
upatikanaji maji kwa wananchi .
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba pamoja na ujumbe
wake, akiwa katika kikao kilichojadili hali ya huduma ya maji kwa
wananchi na namna yakutatua changamoto katika Mamlaka ya Maji Muleba
(MLUWASA) . Wa pili kulia ni Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji Muleba
(MLUWASA) Pontian Thomas.
No comments :
Post a Comment