Mkurugenzi
wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema
Lugangira na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Kituo
cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable
Center,Dk.Gabriel Rugalema,wakionyesha mkataba huo baada ya kuusaini.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema
Lugangira ,akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano na Kituo
cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable
Center,jijini Arusha,leo Oktoba 5,2020
Mkurugenzi
wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema
Lugangira,akisaini mkataba wa ushirikiano na Mkurugenzi wa Kanda ya
Afrika Mashariki na Kusini wa Kituo cha Utafiti wa mbogamboga na matunda
cha Kimataifa cha World Vegetable Center,Dk.Gabriel Rugalema,leo jijini
Arusha,unaolenga kuhamasisha ulaji wa mbogamboga na matunda kama sehemu
ya kuimarisha lishe bora
Mkurugenzi
wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Kituo cha Utafiti wa
mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable
Center,Dk.Gabriel Rugalema,akimkabidhi sehemu ya paketi 500 za za mbegu
bora za mboga mchanganyiko zenye viini lishe, Mkurugenzi wa Shirika
lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema Lugangira.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema
Lugangira na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Kituo
cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable
Center,Dk.Gabriel Rugalema wakiwa kwenye picha ya pamoja huku
wakionyesha mkataba huo baada ya kuusaini.
Na MWANDISHI WETU-ARUSHA
MKURUGENZI
wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema
Lugangira ,leo (Oktoba 5,2020),amesaini mkataba wa makubaliano kati ya
shirika hilo na Kituo cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa
cha World Vegetable Center,utakaosaidia kuboresha lishe.
Shirika
la Agri Thamani lililojikita kwenye kuchangia kutokomeza udumavu na
utapiamlo lenye makao yake makuu mkoani Kagera,linafanya kazi ya kutoa
elimu ya lishe kwenye shule,kaya na jamii na kuhamasisha kilimo lishe.
Mkataba
huo wa makubaliano umesainiwa jijini Arusha ambapo makubaliano hayo
yapo kwenye maeneo saba ikiwemo kuhamasisha ulaji wa mbogamboga na
matunda kama sehemu ya kuimarisha lishe bora na kuwezesha kutokomeza
udumavu na utapiamlo.
Akizungumza
wakati wa tukio hilo,Neema ambaye pia ni Mbunge Mteule wa Viti
Maalum(CCM),Kundi la Asasi za Kiraia (NGO’s),Tanzania Bara,alisema
katika mkataba huo wa miaka mitano wanatarajia kuanza kuutekeleza katika
mikoa saba hapa nchini.
Alitaja
mikoa hiyo ni Kagera,Tanga,Kigoma,Dodoma,Geita,Tabora na Kigoma,ambapo
wanatarajia kuanzisha bustani za mboga lishe za mfano katika Shule zote
za Msingi na Sekondari za Serikali katika mikoa hiyo ambayo itaambatana
na elimu kuanzia kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Alisema
kuwa wanatarajia kuanza zoezi hilo la kuanzisha bustani hizo mwezi huu
katika Manispaa ya Bukoba,ambapo baada ya kumaliza katika halmashauri
hiyo wataanzisha bustani hizo katika shule zingine za mikoa hiyo saba.
“Tutaanzisha
bustani za mboga lishe za mfano kwenye shule zote,watoto chini ya umri
wa miaka mitano,wazee na wenye uhitaji mkubwa wa lishe.Na tumeamua
kuchagua mikoa hii kwa sababu inaongoza kwa changamoto ya ulaji wa mboga
na matunda uko chini,”alisema
Awali
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa kituo
hicho,Dk.Gabriel Rugalema,alitaja maeneo mengine waliyoingia makubaliano
ni pamoja na kueneza elimu ya kilimo na lishe kwa jamii,kuweka msukumo
katika ulaji wa mboga na matunda,kusaidia kuanzisha bustani za mboga na
matunda shuleni.
Nyingine
ni kusaidia kutunga sera na mipango kazi ya Taifa rafiki kwa tasnia ya
kilimo cha mbogamboga na lishe,kuwafikia na kuhamasisha waandishi wa
habari kama wadau maalum wa kusaidia na kueneza elimu ya lishe na
kuangazia akina mama na vijana katika uzalishaji wa mazao ya mbogamboga.
Aidha
Kituo hicho kilitoa pakiti 500 za mbegu za mbegu bora za mgoga
mchanganyiko zenye viini lishe ambazo ndizo zitaanza kwenda kutumika kwa
ajilli ya bustani hizo za mfano katika mikoa hiyo ambayo inaanza
kutekeleza makubaliano hayo.
“Tutashirikiana
kutafuta wadau wengine ambao tutashirikiana nao ili tuweze kufanikisha
hili kwani tumeona ni la muhimu ndiyo maana tumekubali kushirikiana
nao,tunaamini ukipeleka elimu hii kwa wakulima wa kawaida utajenga uwezo
wao wa lishe na kiuchumi kwani Tanzania ina chakula lakini haina lishe
bora,”alisema Dk. huyo.
No comments :
Post a Comment