Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt Maduhu Kazi amekadhi serikalini shule mbili zilizojengwa na mwekezaji wa Alliance Ginnery katika vijiji vya Salama na Bugatu kwa upande wa Sekondari na Kijiji cha Kasoli kwa upande wa chuo cha ufundi stadi.
Shule hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Salum Kali ambaye alipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka kwa upande wa shule ya ufundi.
Dkt. Maduhu Kazi amewapongeza wawekezaji hao kwa moyo wao wa kurudisha shukran kwa wananchi kwa kufanya maendeleo kwa wananchi.
Dkt.
Kazi amesema TIC inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wawekezaji kwa
nchi na jamii kwa ujumla na hivyo na serikali itaendelea kuvutia
uwekezaji ili kuendelea kutoa chachu ya maendeleo kwenye maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Naye Mh. Mtaka amemshukuru Mwekezaji na kusema Mwekezaji huyu ni wa kipekee na amekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya vijiji vingi vya Simiyu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magu amemshukuru Mwekezaji na kusema kuwa
watahakikisha wanafanya taratibu za usajili haraka ili shule isajiliwe
mapema na kuanza kupokea wanafunzi ili kuanza sasa kutumika kama shule.
No comments :
Post a Comment