Wananchi
wakipata maelezo ya ufugaji bora wa samaki kutoka kwa Afisa Uvuvi
Mwandamizi, Nelson Mbawala wakati wakitembelea mabanda ya Wizara ya
Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula
Duniani yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mjimwema kitaifa mkoani Njombe
tarehe 10-16, Oktoba 2020.
Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Elifatio towo
(Kulia) akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Maadhimisho
ya kitaifa ya Siku ya Chakula duniani Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba
(kushoto) muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la taasisi hiyo leo
(10.10.2020). Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi)
Dkt.Rashid Tamatamah.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt.Rashid Tamatamah
akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo (10.10.2020)
kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani
uliofanyika Mkoani Njombe.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt.Rashid Tamatamah (kulia)
akifafanua jambo kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya
Chakula duniani ambaye pia Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba
(kushoto) kufika katika banda hilo leo (10.10.2020)
No comments :
Post a Comment