Thursday, October 8, 2020

TANESCO DODOMA YASHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUBORESHA HUDUMA ZAO


Meneja Mahusiano wa TANESCO ,Johary Kachwamba akizungumza na wateja waliofika katika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja kwa kukata keki pamoja na wateja hao.

Meneja Mahusiano wa TANESCO ,Johary Kachwamba akiwa pamoja na wateja  waliofika katika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja kwa kukata keki pamoja na wateja hao.

 

‘Meneja Mahusiano wa TANESCO ,Johary Kachwamba akifurahia jambo na wateja walioweza kukata Keki kwa pamoja  katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja.

  

Sehemu ya wateja mkoa wa Dodoma wakifatilia tukio la kukata keki wakati  kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja kwa kukata keki pamoja na wateja hao.

Meneja Mahusiano wa TANESCO Johary Kachwamba akimshuhudia mteja akikata keki wakati wa kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja.

Meneja Mahusiano wa TANESCO ,Johary Kachwamba akiwalisha keki baadhi ya wateja waliofika katika Ofisi za Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja.

Meneja wa Mkoa Dodoma Frank Chambua akimlisha Keki Mteja aliyefika katika Ofisi hizo kwa ajili ya  kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja .

Picha ya pamoja mara baada ya kukata keki katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

 

Meneja Mahusiano wa TANESCO ,Johary Kachwamba akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukata keki na kuwalisha wateja waliofika katika ofisi hizo kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja .

Muonekano wa jengo la Ofisi za TANESCO Mkoa wa Dodoma

……………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  limeadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja kwa

kusogeza huduma karibu zaidi kwa wateja wake katika mkoa wa Dodoma kwa kujumuika nao na kukata keki kwa pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo.

Meneja Mahusiano wa TANESCO ,Johary Kachwamba amesema kuwa TANESCO inawathamini Wateja wake  ndio maana wameamua kukata keki kwa pamoja.

Bi.Johary amesema kuwa anawashukuru wateja kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya TANESCO hivyo wataendelea kuboresha na kutatua changamoto katika huduma zao.

”Tunawaahidi wateja wetu mliofika na kujumuika na sisi siku ya leo tunatoa ahadi ndani ya masaa 24 wateja wetu mtukuwa mmepata huduma kutoka kwetu”amesema Bi.Kachwamba

Bi.Kachwamba amesema kuwa  pamoja na uwepo wa Wiki ya huduma kwa Wateja TANESCO wataendelea kutoa huduma iliyotukuka kwa wateja wao kabla, wakati na baada kuhitaji huduma zao  ili kukidhi kiwango na matarajio ya mteja.

“Katika kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma kwa wakati TANESCO tumeendelea kubuni njia mbalimbali ambazo wateja wetu wanaweza kuuliza, kutoa maoni na kero mbalimbali na kuweza kujibiwa na watoa huduma wetu kwa haraka zaidi”. Amesema Bi.Kachwamba

 

No comments :

Post a Comment