Thursday, October 1, 2020

TAKUKURU DODOMA YAOKOA BILIONI MOJA NA KUZIREJESHA SERIKALINI NA VYAMA VYA USHIRIKA

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma ,Sosthenes Kibwengo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa kuhusu taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021 ya taasisi hiyo leo jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma imeokoa zaidi ya shilingi bilioni moja pamoja na kuzirejesha Serikalini  na kwenye vyama vya Ushirika.

Aidha katika  fedha hizo sh.milion 323.681,100 ambazo zinajumuisha fedha walizolipwa

wakandarasi kinyume na mikataba. 

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma ,Sosthenes Kibwengo,wakati akitoa taarifa kwa  waandishi wa habari  kuhusu taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021 ya taasisi hiyo.
 Kibwengo amesema kuwa katika  fedha hizo zilikusanywa kutoka katika malipo ya watumishi wa umma,madeni,Saccos na za mikopo umiza.. 
Hata hivyo Kibwengo ametoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo kuwa kiasi cha sh.Milioni  81 zimereshwa na wakandarasi na watumishi wa TARURA waliolipwa bila kustahili. 
“Takukuru imefanikiwa pia kurejesha viwanja sita vyenye thamani ya sh milion 72 waliokuwa wamedhulumiwa haki yao, “amesema  Kibwengo. 
Fedha zilizorejeshwa kuanzia Juni 2020 zimefikia sh 104,460,557 kati ya sh. 124,514,024 zinazopaswa kurejeshwa. 
Aidha Kibwengo amesema kuwa kuna fedha pia ambazo zimerejesha sh milion 18 za mstaafu ambaye mwaka 2016 alizotoa kwa kampuni moja ili apewe trekta Kisha kampuni hiyo kushindwa kutimiza . 
Kibwengo alifafanua zaidi ya kuwa sh. milioni 950,300,000 ziliokolewa na ushirikiano na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa serikali baada ya kufanya uhakiki wa ndani na kwenye jedwali ya fidia kwa wananchi waliotwaliwa ardhi zao kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko wa nje jijini Dodoma. 
“Katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inafanyika kwa weledi na thamani halisi ya fedha inapatikana tumekagua miradi 19 yenye thamani ya zaidi ya sh bilion 6
Aidha katika sekta ya za Maji, Ujenzi  afya na Elimu ambapo hatua mbalimbali zilikuwa zimechukuliwa ikiwemo kutolewa maelekezo ya marekebisho ya baadhi ya dosari”amesisitiza
Kibwengo ameongeza kuwa wao wakiwa mabalozi wa kupambana na vitendo vya rushwa ,wanaendelea na uchunguzi wa shilingi milioni 245 baada ya viashiria vya jinai kuonekana katika miradi miwili ya maji wilayani Kongwa yenye thamani ya sh 1,538,417,421.
Amezitaja  sekta zinazoongoza kulalamikiwa na Wananchi kuwa ni  Ardhi  kwa asilimia 60,ikifuatiwa na vyama vya Siasa kwa asilimia12,huku Ujenzi ikiwa na asilimia tano, mikopo Umiza asilimia tano na polisi asilimia nne. 
Kibwengo amesema kuwa wameweza kupokea taarifa 482 za rushwa, na wamekamilisha uchunguzi wa majalada 16 na kufungua mashauri 15.
“Tumefanya uchambuzi wa mifumo ya utendaji na utoaji huduma katika sekta ya kodi,afya na fedha za kuendesha warsha,”ameongeza

No comments :

Post a Comment