*WAADHIMISHO YA MIAKA 146 YA POSTA
………………………………………………………………………
Na .Mwandishi wetu
Katika kuadhimisha miaka 146 ya Posta duniani, Shirika la Posta limewaasa Watanzania kutumia huduma ya Posta kwa ajili ya maendeleo ya nchi ikiwemo kutoa huduma ndani na nchi
192 duniani.Shirika Posta nchini limefanya maadhimisho hayo na kuweka wazi mikakati yake ya kutumia teknolojia ya kisasa ili kuongeza ufanisi kwenye kazi zao na kuwahudumia watanzania wote.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar Es Salaam, katika maadhimisho ya miaka 146 ya posta duniani, Posta Masta Mkuu wa shirika hilo,Hassan Mwan’gombe Shirika limeweza kupata faida kubwa na kuweza kutoa gawio la serikalini Milioni 350 kutokana na mfumo wa kidijitali.
Mwang’ombe amesema mfumo wa Kidijitali umeweza kuwasaidia na. kuboresha shughuli za shirika hilo ndani na nje ya nchi na kujiinua kiuchumi na kupata faida kubwa.
Amesema, Shirika linafanya huduma ya kusafirisha mizigo nchi 192 ambazo zinapata huduma hiyo na limeweza kuhakikisha mizigo ya wateja inafika kwa usalama mkubwa na uaminifu.
Aidha, Mwang’onde ameeleza Shirika la Posta lipo mbioni kuzindua huduma ya Posta mkononi kama njia ya kuwarahisishia wateja wao kupata huduma popote waliopo.
“Wateja watajisajili kwa njia ya simu na kwa sasa hivi mteja hatajihitaji kufuata barua yake katika sakundu la Posta bali itamfuata alipo.”
Amesema, Posta ni zaidi ya barua kwani wanasafirisha bidhaa mbalimbali wana magari yanayosafirisha vitu nchi nzima na pia wana mpango wa kuwa na boti yao ili kurahisisha usafiri wa mizigo.
Akielezea kwa kina kuhusiana na huduma ya Posta wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona, Mwa’gombe amesema “katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya COVID 19 serikali ilitupatia jukumu la kusafirisha sampuli kutoka eneo moja hadi na tulifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa sana.”
Nakuongeza kuwa Shirika hilo lilikuwa miongoni mwa kudhibiti janga hilo.
Pia baada ya mkutano huo kulifanyika ziara fupi ya kutembelea baadhi ya vitengo vinavyotoa huduma ya kusafirisha na kupokea mizingo ya wateja.
No comments :
Post a Comment