**********************************
NJOMBE
Licha ya Tanzania kuwa
mzalishaji mkubwa wa Nyama na Maziwa lakini inaelezwa bado kuna kiwango
kidogo zaidi cha matumizi ya vyakula hivyo ambavyo muhimu zaidi katika
kujenga afya ya binadamu.
Akitoa takwimu za
serikali Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Rashid Tamatamah
amesema katika kipindi cha mwaka 2019/20 Tanzania imezalisha maziwa bil 3
wakati mwaka wa nyuma ikizalisha lita bil 2 hatua ambayo inatajwa
kuchangiwa na ongezeko la Ng’ombe pamoja na maboresho makubwa
yaliofanywa na serikali katika ya mifugo,uvuvi na kilimo.
Kuhusu zao la Nyama
Tamatamah pia amesema kuna ongezeka la uzalishaji kutoka tani laki 6.9
zilizozalishwa mwaka 2018/19 hadi tani laki 7.16 katika mwaka wa
serikali 2019/2020 jambo ambalo limekuwa na matokeo chanya katika kukuza
uchumi wa nchi huku pia akiwataka wananchi kujenga utamaduni wa kula
vyakula bora kwa kuzingatia kanuni za lishe ili kuepukana na changamoto
ya udumavu wa akili na maarifa.
“TNchi yetu inazalisha
kiwango kikubwa cha maziwa na Nyama lakini cha kushangaza bado watu
wanachangamoto ya udumavu hivyo tuanze kujenga utamaduni wa kunywa
maziwa na nyama ili kukidhi mahitaji ya mwili kwa mujibu wa shirika la
chakula duniani” Alisema Dkt Tamatamah .
Katika hatua nyingine
Kaimu Mkurugenzi huduma, wizara ya Mifugo na Uvuvi idara ya Utafiti
mafunzo na huduma za ugani Dkt Kejer Gillah amesema Watanzania Wengi
wamekuwa na hawali vyakula vyenye protini ya daraja la kwanza kama vile
nyama na samaki jambo ambalo limekuwa changamoto katika makuzi ya watoto
na afya bora ya akili.
Dkt Gillah anasema
njia pekee ya kuepukana na udumavu ni kuzingatia mlo wa makundi yote ya
chakula na kudai kwamba ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema
serikali kupitia wizara ya kulimo na uvuvi imekuwa ikifanya tafiti
mbalimbali za vyakula vinavyofaa kwa matumizi ya binadamu.
“Idadi kubwa ya
watanzania wanakosa vyakula vyenye protein ya daraja la Kwanza jambo
ambalo limekuwa na athari katika afya ya akili na kwamba kupitia
maonyesho hayo wizara inatumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma”Alisema
Dkt Kejeri Gillah.
Kwa upande wao baadhi
ya wakazi wa Njombe ambao wamejitokeza katika viwanja vya maonyesho
Akiwemo Titho Mng’ong’o wanasema wamefurahishwa na kitendo cha serikali
kuupa heshima mkoa wa Njombe kuwa mwenjeji wa maonyesho hayo kw kuwa
wameweza kupatiwa elimu mbalimbali za lishe pamoja na kupewa ujuzi wa
matumizi ya teknolojia mbalimbali za kilimo.
“Tunashukuru kupitia
maonyesho haya tumeweza kujifunza mambo mengi ambayo yanafaida kwetu na
kwamba tunakwenda kuyafanyia kazi ipasavyo”,Alisema Titho Mng’ong’o
No comments :
Post a Comment