Wednesday, October 7, 2020

RAIS MHE.DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA MALAWI DKT. LAZARUS CHAKWERA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati nyimbo za Mataifa mawili ya Tanzania na Malawi zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera akifurahia jambo wakati akiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba 2020. PICHA NA IKULU

 

No comments :

Post a Comment