Meneja
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Njombe, Mrisho
Mwisimba (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa
Sylvester Mpanduji aliyetembelea banda la NSSF katika maonesho ya Siku
ya Chakula Duniani yanayoendelea mkoani Njombe. SIDO kwa kushirikiana na
NSSF, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), VETA na benki ya
Azania kwa pamoja wanaratibu mpango wa kuendeleza viwanda vidogo na vya
kati (SANVN VIWANDA SCHEME) ambapo tayari NSSF imeshatoa bilioni 5, huku
SIDO na VETA wanahusika na utambuzi wa wajasiriamali, NEEC kazi yake ni
kuratibu mpango huo na benki ya Azania inahusika kutoa mikopo hiyo.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba(kulia) akimpa maelezo Kaimu
Katibu Mkuu wa Wiraza ya Kilimo, Dkt. Honest Kessy
(Kushoto)alipotembelea maonesho ya Nane ya Siku ya Chakula Duniani
yanayofanyika katika viwanja vya Mji Mwema mkoani Njombe.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba akizungumza katika maonesho ya
Nane ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mji
Mwema mkoani Njombe, ambapo amewahimiza wananchi kujiunga na Shirika
hilo ili wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF
No comments :
Post a Comment