Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka, akizungumza na waandishi wa
habari leo wakati akitangaza kuwa chuo hicho kinatarajia kuanza ujenzi
wa tawi lake jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Prof.Eliamani Sedoyeka, akisisitiza jambo kwa na waandishi wa habari
leo wakati akitangaza kuwa chuo hicho kinatarajia kuanza ujenzi wa tawi
jipya jijini Dodoma kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango Benny Mwaipaja.
Sehemu ya waandishi wa habari
wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani
Sedoyeka,(hayupo pichani)wakati akitangaza kuanza kwa ujenzi wa tawi
jipya la chuo hicho jijini Dodoma.
Maafisa kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha wakifatilia Mkutano huo.
Mipango Benny
Mwaipaja,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma wakati
Chuo cha Uhasibu Arusha kinatangaza kuanza ujenzi mpya wa tawi lake.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa chuo
hicho mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa
chuo hicho jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa
habari mara baada ya kuzungumza nao kuhusu ujenzi wa chuo hicho jijini
Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Na Alex Sonna ,Dodoma
CHUO cha Uhasibu
Arusha(IAA), kinatarajia kufungua tawi lake Jijini Dodoma Desemba mwaka
huu kwa ajili ya masomo ngazi ya shahada ya uzamili na mafunzo ya muda
mfupi kwa mawakala wa benki na wanaoendesha huduma za fedha kwa njia ya
simu.
Akizungumza leo na
waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkuu wa Chuo hicho, Prof.Eliamani
Sedoyeka, amesema kitaanza kutoa masomo hayo kwenye jengo la kupanga
huku wakitarajia kuanza ujenzi wa majengo yao Januari 2021 kwenye eneo
la Njedengwa.
Amesema kuwa hatua
hiyo inatokana na nusu ya wanafunzi wa shahada ya uzamivu kuwepo Dodoma,
hivyo Chuo kinafungua tawi hilo ili kurahisisha utoaji elimu na kuunga
mkono jitihada za serikali kuhamia Dodoma.
Prof.Sedoyeka amesema watajenga kwa kutumia utaratibu wa ‘force account’ ili kuanza kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya astashahada.
Kuhusu mafunzo ya
muda mfupi, Mkuu huyo amesema yatatolewa kwa wiki sita na yanalenga
kuchochea masuala ya kiuchumi ili kuwepo na uchumi shirikishi wenye
weledi na ujuzi.
Amebainisha kuwa
katika Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya Fedha nchini wa miaka 10,
Taasisi za elimu ya juu nchini na taasisi za utafiti zimeagizwa kutumia
fursa zilizo kwenye mpango huo ili kujipanga katika kuboresha maeneo ya
kitaalamu na kiutafiti ili sekta iendelee kukua na kuhimilia ushindani
na mabadiliko.
“Kwenye Mpango kuna
maagizo kwenye taasisi za elimu ili kufanikisha kufikia malengo hayo,
tukaamua kuanzisha course za muda mfupi ambazo zitakuwa za wiki sita kwa
Agent Banking na Mobile money kutokana na sekta hii ndio inaonekana
kukua kwa kasi lakini watoa huduma hawana utaalam huo,”amesema.
Amesema sekta hiyo
inakua kutokana na uwekezaji wa serikali kwenye masuala ya mawasiliano
na upatikanaji wa umeme ambapo huduma hizo zipo hadi maeneo ya vijijini
hivyo mafunzo hayo yatakuwa ya muhimu kwao kuwa wabobezi kwenye utoaji
wa huduma hiyo.
“Ili kuendana na
jitihada za serikali tumejipanga kutoa mafunzo haya ambayo yatawafikia
moja kwa moja watanzania, hii sekta ndogo ya fedha sio ndogo kama
tunavyofikiri ndio eneo ambalo watanzania wengi kwasasa wanatumia,
tunaamini hatua hii itasaidia kutambua biashara hiyo lakini pia kujua
namna ya kuiendesha,”amesema.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo kwasasa yatatolewa Arusha, Dar es salaam na Dodoma na baadaye yataenda kwenye maeneo mengine.
No comments :
Post a Comment