Kamishina
wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Balozi Omari Ramadhani Mapuri
akizungumza mbele ya Watazamaji wa Uchaguzi Mkuu 2020 wa Ndani na NJe ya
Tanzania jijini Dar walipokuwa wakielezwa matayarisho ambayo imefanya
na yale ambayo inaendelea kuyafanya na kwa kiasi kile ambacho Tume
imejiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba
28,2020 nchini kote.Picha na Michuzi JR-MMG.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza mbeleya viongozi
Waandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Watazamaji wa Uchaguzi
Mkuu 2020 wa Ndani na NJe ya Tanzania,namna Jeshi la Polisi
lilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.
Sehemu ya meza kuu ya Viongozi Waandamizi wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), wakifuatilia yaliyokuwa yakielezwa ukumbini humo.
Baadhi
ya Watazamaji wa uchaguzi kutoka nje na ndani ya Tanzania wakifuatilia
yaliyokuwa yakielezwa na Tume ya Uchaguzi kuhusu namna ilivyojiandaa
kuhakikisha uchaguzi unakuwa Huru na wa Haki na kwa utulivu mkubwa.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Simon Sirro akifuatilia mambo mbalimbali
yaliyokuwa yakielezwa na Tume ya Uchaguzi katika kikao hicho muhimu cha
kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa utulivu mkubwa.
Watazamaji
kutoka Nje ya Nchi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi,namna ilivyojiandaa kufanikisha shughuli nzima ya Uchaguzi Mkuu
2020,unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020 nchini.
Baadhhi
ya Watazamani wa ndani wa Uchaguzi wakichangia mawazo yao katika
kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa Amani na utulivu nchini.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Simon Sirro akifafanua jambo kwenye kikao
hicho kilichowakutanisha watazamaji wa uchaguzi kutoka nje na ndani ya
Tanzania ,ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa ikieleza matayarisho
ambayo imefanya na yale ambayo inaendelea kuyafanya na kwa kiasi kile
ambacho Tume imejiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imekutana na watazamaji wa uchaguzi
kutoka nje na ndani ya Tanzania kuelezea matayarisho ambayo imefanya na yale ambayo inaendelea kuyafanya na kwa kiasi kile ambacho Tume imejiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo.NEC
imekutana na watazamaji hao ambapo pamoja na mambo mengine watazamaji
hao wameelezea kufurahishwa na maandalizi yanayoendelea kufanywa kwa
ajili ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka
huu.
Watazamaji
hao wamezungumzia pia mchakato huo wa NEC ambavyo umekuwa wa uwazi kwa
watu wote ambao umeendelea mpaka sasa na suala kubwa lilikuwa ni
kuendelea kuwahimiza watu kuzingatia sheria, wazingatie taratibu ili
siku hiyo ya uchaguzi watakapoenda kupiga kura kwa wamani.
Akizngumza
mbele ya watazamaji hao, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria NEC Emmanuel
Kawishe amefafanua kwamba watazamaji wenyewe wamesisitizana kufuata
sheria , kuzingatia miongozo iliyotolewa na Tume ili uchaguzi uendelee
kuwa wa amani maana kuna maisha baada ya uchaguzi.
"Wawakilishi
wa taasisi zote za kimataifa ambazo ziko 17 na tunawawakilishi kutoka
taasisi za ndani ambazo ni 97, tumekuwa na wawakilishi kutoka kila
taasisi na kila moja imeleta wawakilishi zaidi ya wawakilishi wanne.Pia
tulikuwa na Rais mstaafu wa taifa la Burundi ambaye naye alikuwa katika
misheni yetu tuliyokuwa nayo hapa,"amesema Kawishe.
Kwa
upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema
unapokuwa mtazamaji haina maana unaweza kuwa juu ya sheria na kwamba
unaweza kutoka nje lakini usipofuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na usipofuata sheria ambazo zipo hapa nchini unaweza kujikuta
unakuwa muhalifu na sheria itachukua mkondo wake.
"Kwa
hiyo nilikuwa nasisitiza suala hilo kwamba pamoja na kuwa waangalizi
hao ni wageni kwa ajili ya kutazama uchaguzi ambao tunatarajia kuufanya
lakini ni vema wakajitahidi kutovunja sheria kwani wakizivunja sheria
itachukua mkondo wake.
"Lakini
nawakumbusha hawa waangalizi au watazamaji wa hapa nchini kwamba
tumeshapewa hii nafasi basi serikali imeona unafaa kuwa mtazamaji , basi
kikubwa ni kwamba usivunje sheria ,na jaribu sana kuhakikisha wanatenda
haki ,wanashauri jambo ambalo ni la haki wasiingie tena katika mambo ya
ushabiki , kwani wakishaingia katika ushabiki mwisho wa siku unajikuta
umeingia kwenye uhalifu na tutashughulika kama tunavyoshughulikia
wahalifu wengine,"amesema IGP Sirro.
Amesisitiza
cha msingi mazungumzo yalikuwa mazuri kati yao wadau na NEC , kwani
wamekumbushwa kuzingatia wajibu wao , jeshi limekumbusha wajibu wao na
watazamaji nao wamekumbushwa kutimiza wajibu wao , hivyo amepata faraja
kuona kila mdau ametakiwa kutimiza wajibu wake.
No comments :
Post a Comment