Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amiepongeza Benki ya
CRDB kwa kuchukua hatua ya kuifufua Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL)
na hivyo kutoa tumaini jipya kwa vyama vya ushirika nchini ambao ni
wadau wakubwa wa benki hiyo. Naibu Waziri Kijaji ametoa pongezi hizo
katika hafla ya uzinduzi wa huduma za Benki ya Ushirika Kilimanjaro
(KCBL) iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo mkoani Kilimanjaro
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania, Dkt. Benard Kibese.
Nae
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Benard Kibesse ameipongeza
Benki ya CRDB kwa uwekezaji huo na kusema kuwa benki nyingi nchini
hazikua tayari kuwekeza katika benki hiyo lakini Benki ya CRDB iliweza
kuchukua uamuzi huo kutokana na yenyewe kuwa ni zao la ushirika kama
ilivyo Benki ya KCBL. Dkt. Kibese amesema pamoja na uwekezaji huo kwa
Benki ya CRDB lakini haifanyi kuwa Benki ya KCBL kuwa mali ya Benki ya
CRDB bali benki hiyo itabaki kuwa ya ushirika kama dhamira ya kuianzisha
ilivyokua.
Naibu
Waziri Kijaji amesema kuwa ushirika ni sehemu ya utekelezaji wa
vipaumbele vya Dira ya Maendeleo ya Taifa na Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dokta John Pombe Magufuli imejidhatiti katika
kuhakikisha mwelekeo wa jumla wa Ushirika katika siku za usoni
unaiongoza jamii ya Watanzania kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
“Kama
Naibu Waziri mwenye dhamana ya sekta ya fedha nchini nimefurahishwa
sana na uamuzi huu wa Benki ya CRDB kuweka mtaji katika Benki hii ya
KCBL ambayo kwetu sisi tunaitazama kama Benki Kuu ya Ushirika katika
siku za usoni na ni imani yangu kuwa uwekezaji huu utakwenda kuifanya
Benki ya KCBL kuwa na ushindani zaidi kwenye soko na hivyo kuleta tija
sio tu kwa Serikali bali kwa Watanzania kwa ujumla” alisema Naibu Waziri
Kijaji.
Naibu
Waziri Kijaji amewasihi watendaji wa Benki ya KCBL kuhakikisha kuwa
wanakwenda kusimamia vyema rasilimali na benki hiyo na kutokua na mchezo
na wote ambao wanaonyesha kutokua na nia njema na benki hiyo ili
kutoirudisha benki hiyo ku. Sambamba na hilo Waziri Kijaji ameiomba
Benki ya KCBL kuweka mikakati ya kutoa elimu kwa wateja ili kuchochea
upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wengi zaidi hususan
ambao wapo kwenye ushirika.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki
ya CRDB na , Bw. Fredrick Nshekanabo amewaomba wateja, vyama vya
ushirika, akiba na mikopo, na wadau wote wa KCBL kurejesha imani kwa
benki hiyo kwani sasa Benki ya CRDB inakwenda kuirejesha kwenye ramani
kupitia uwekezaji wa mtaji pamoja na rasimali watu. Kaimu Mkurugenzi
huyo amesema kuwa wanaamini uzoefu wa Benki ya CRDB katika masuala ya
ushirika kutokana na chimbuko lake kuwa kwenye ushirika utakua chachu
kubwa katika kuifufua benki hiyo kama ambavyo wameweza kufanya kwa Benki
ya TACOBA ambayo ilipitia kipindi kigumu kama ilivyo kwa Benki ya
Ushirika Kilimanjaro na sasa inafanya vizuri na kupata faida.
“Siku
zote ahadi yetu kwa serikali ni kuwa “TUPO TAYARI” kushiriki katika
utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa ajili ya ustawi wa
nchi yetu ya Tanzania. Na leo naomba kurudia tena kuwa “TUPO TAYARI”
kuhakikisha tunairudisha KCBL kwenye ramani na kuipa sura mpya ambayo
itakua na tij kwa wadau wake wote. Nakuomba utufikishie salamu kwa Mh.
Rais kuwa jambo hili la KCBL tumelichukua na kwa lugha ya sasa tunasema
hili ni “JAMBO LETU” na tutakwenda nalo ije mvua lije jua hadi
kulifanikisha” alisema Nshekanabo.
Katika
uwekezaji huo Benki ya CRDB imewekeza mtaji wa Shilingi Bilioni 7 ili
kuongeza mtaji na ukwasi kwa Benki ya KCBL ambayo ilipitia kipindi
kigumu kifedha kutokana na ubadhilifu wa baadhi ya watendaji wake na
kupelekea benki hiyo kusimamisha shughuli za uendeshaji. Sambamba na
mtaji huo Benki ya CRDB itatoa rasilimali watu ili kusimamia uendeshaji
wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro ambapo Benki ya CRDB itatoa watendaji
wanne katika nafasi za nafasi za Meneja Mkuu, Mkuu wa Idara ya Fedha na
Uendeshaji, Mkuu wa Idara ya Mikopo na Ukuzaji wa Biashara pamoja Mkuu
wa Idara ya Ukaguzi wa Ndani pamoja na wajumbe wawili wa Bodi.
Kuhusu Benki ya CRDB
Benki
ya CRDB ni moja benki zinazoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki,
inatoa huduma kwa wateja wadogo, wakati na wakubwa ikiwamo huduma kwa
wateja binafsi, huduma za hazina, huduma za bima, mikopo ya biashara,
kilimo na uwezeshaji kwa wajasiriamali wadogo.
Benki
ya CRDB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kutambuliwa na kampuni ya
kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kuwa moja kati ya
benki 10 imara na salama Afrika katika uwekezaji. Moody’s imeipa Benki
ya CRDB daraja la uimara la B1 ambapo ni daraja la juu zaidi kupatikana
kwa mabenki na taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara.
Benki
ya CRDB imekuwa kiungo muhimu cha biashara katika nchi za Tanzania na
Burundi kwa kuwahudumia wateja zaidi ya milioni 3 na kupitia mtandao
mpana wa matawi 268, zaidi ya CRDB Wakala 15,000, 537 ATM, mashine za
manunuzi 1,200 na Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa
24/7.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Jina
Namba ya Simu
Barua Pepe
TullyEsther Mwambapa
+255 769 200 600
No comments :
Post a Comment